Lengo
Kusimamia na kushauri masuala yote yanayohusu miundombinu katika Halmashauri. Majukumu Kitengo kitafanya kazi zifuatazo:-
1.Kushauri kuhusu masuala ya sekta ya ujenzi;
2.Kupanga maendeleo ya miundombinu;
3.Kuchambua na kutoa mapendekezo ya madai ya malipo ya wakandarasi;
4.Kukagua kazi za ujenzi zinazofanywa na Halmashauri na kuhakikisha ubora wake;
5.Kutoa vyeti kwa wakandarasi kwa mikataba iliyokamilika;
6.Kufanya uwekaji lami wa barabara mpya kwa kushirikiana na TARURA;
7.Kuanzisha na kudumisha ushirikiano na Taasisi za nje na ndani ya Nchi zinazoshughulikia masuala ya miundombinu;
8.Kushiriki katika kuwezesha utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi;
9.Kusimamia mchakato wa ukuaji wa miji kwa kushirikiana na Wizara yenye dhamana ya ardhi; na
10.Kusimamia maendeleo ya makazi vijijini na mijini kwa kushirikiana na Wizara yenye dhamana ya Ardhi.
Kitengo hiki kitaongozwa na Mkuu na kitajumuisha Sehemu tatu (3) kama ifuatavyo:-
(i) Sehemu ya Kazi;
(ii) Sehemu ya Barabara; na
(iii) Sehemu ya Maendeleo Vijijini na Mijini.
3.1.1 Sehemu ya Kazi
Kitengo kitafanya shughuli zifuatazo:-
1.Kutoa ushauri wa sheria, kanuni, taratibu na mambo yote yanayohusu ujenzi;
2., kutafsiri na kusimamia utekelezaji wa sera, sheria na kanuni za masuala ya ujenzi;
3.Kuandaa mikataba inayohusiana na majengo na mitambo;
4.Kutayarisha na kukadiria gharama za ujenzi;
5.Kufuatilia utendaji kazi wa wakandarasi;
6.Kuchambua na kutoa mapendekezo ya madai ya malipo kutoka kwa wakandarasi;
7.Kukagua majengo na kuhakikisha ubora wake;
8.Kutoa hati kwa wakandarasi kwa kazi zilizokamilika kulingana na mikataba; na
9.Kusimamia uendeshaji wa warsha za Halmashauri.
Sehemu hii itaongozwa na Afisa Mfawidhi.
Kitengo kitafanya shughuli zifuatazo:-
1.Kutoa ushauri kuhusu masuala yanayohusiana na utambuzi na uwekaji lami wa barabara mpya;
2.Kuchambua, kutafsiri na kusimamia utekelezaji wa sera, sheria na kanuni kwenye barabara za lami;
3.Kutengeneza barabara mpya katika ardhi iliyopimwa;
4.Kuandaa mikataba ya uwekaji lami wa barabara mpya;
5.Kutayarisha makadirio ya gharama za kuweka lami barabara;
6.Kufuatilia utendaji wa wakandarasi;
7.Kutoa hati kwa wakandarasi kwa kazi zilizokamilika kulingana na mikataba;
8.Kuchambua na kutoa mapendekezo ya madai ya malipo kutoka kwa wakandarasi;
9.Kukagua barabara za lami ili kuhakikisha ubora; na
10.Kusimamia ujenzi na matengenezo ya vituo vya mabasi.
Sehemu hii itaongozwa na Afisa Mfawidhi.
3.1.3 Sehemu ya Maendeleo Vijijini na Mijini
Sehemu hii itafanya shughuli zifuatazo:-
1.Kusimamia maendeleo ya makazi vijijini na mijini kwa kushirikiana na Wizara yenye dhamana ya ardhi;
2.Kusimamia huduma za kimazingira na kijamii;
3.Kuongoza mipango ya maendeleo ya miji, makazi na matumizi endelevu ya ardhi;
4.Kusimamia na kuratibu usimamizi wa mambo ya kale na utalii;
5.Kusimamia mchakato wa ukuaji wa miji kwa kushirikiana na Wizara yenye dhamana ya ardhi;
6.Kuratibu na kukuza maendeleo ya miji inayochipukia kutoka vijiji hadi makazi ya mijini; na
7.Kushiriki katika kuwezesha utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi.
Sehemu hii itaongozwa na Afisa Mfawidhi.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa