1. Kuhakikisha kuwa kuna usawa wa Kijinsia katika jamii katika utekelezaji wa shughuli zote za kiuchumi na kijamii.
2. Kuwezesha jamii kwa kuwapatia mikopo midogo yenye riba nafuu ya 10% kwa vikundi vya kiuchumi vya Wanawake na Vijana ili waweze kujikwamua kiuchumi na kupambana na umasikini.
3. Kusajili vikundi vya kijamii na kuvihamasisha kufungua akaunti katika benki na kujiwekea akiba
4. Kuhamasisha na kuwawezesha wananchi kupanga mbinu za kutatua vikwazo vya maendeleo hasa vya maji na nishati kwa kuwa na miradi ya uvunaji wa maji ya mvua, majiko sanifu na uhifadhi wa vyanzo vya maji
5. Kuwezesha jamii kushiriki katika kubuni, kupanga, kutekeleza, kusimamia, na kutathimini mipango/miradi ya maendeleo
6. Kuhamasisha jamii na kuelimisha jamii kuondokana na mila na desturi zenye kuleta madhara kwa jamii na kuwa na mtizamo wa kupenda mabadiliko na maendeleo
7. Kuhakikisha haki za watoto zinalindwa na kutekelezwa katika jamii.
8. Kutambua watoto waishio katika mazingira hatarishi na kuwapatia misaada.
9. Kuwezesha makundi maalum ikiwemo watu wenye ulemavu
10.Kuratibu na Kuhamasisha jamii kupamabana na kujikinga na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI na UKIMWI.
11. Kuratibu shughuli za miradi ya maendeleo kupitia mradi wa TASAF awamu ya III kwa usaidia kaya masikini
12. Kuhamasisha na kuwawezesha wananchi kupanga na kutekeleza kazi za maendeleo ambazo ni pamoja na usafi wa mazingira, ujenzi wa nyumba bora, ujenzi wa shule, zahanati, majosho, barabara, uchimbaji wa visima vifupi na shughuli zingine zote za maendeleo.
13. Kutafsiri na kusimamia utekelezaji wa Sera na Sheria mbali mbali za Taifa. Sera na Sheria hizo ni Sera ya maendeleo ya Jamii Jinsia na watoto ya Mwaka 2000, Sheria ya Mtoto ya mwaka 1996, 2008, Sheria ya watu wenye ulemavu ya Mwaka 2010 n.k
14. Kushirikisha jamii katika kubuni na kupanga miradi mbali mbali ya Maendeleo.
15. Kuratibu shughuli za Asasi za kiraia na zisizo za kiserikali zinazofanya kazi katika Halmashauri.
16. Pia Idara ni kiungo cha wananchi na wadau mbali mbali wa maendeleo katika shughuli mbalimbali za kuiletea jamii maendeleo.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa