1. Kitengo cha Habari, na Mawasiliano kina jukumu la kuhakikisha Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa inadumisha
mahusiano chanya na wadau wake wa ndani na nje.
2. Kutangaza shughuli zote za serikali na kuujulisha umma shughuli za maendeleo zinazotekelezwa katika Halmashauri ya Manispaa
kwa njia mbalimbali zikiwemo magazeti, majarida,vitabu, vipeperushi, radio, TV na tovuti.
3. Majukumu mengine ya msingi ya Kitengo yanahusu kusimamia,kuratibu na ushauri wa matumizi ya teknolojia ya kompyuta.
Kusimika Mfumo wa Kompyuta wa Kuhifadhi taarifa na Kumbukumbu za Watumishi na Mishahara (Intergrated
Human Capital Management System); pamoja na utekelezaji wa Sera ya Serikali Mtandao (e-government policy) katika utumishi
wa umma
4. Aidha, Ofisi hii ina jukumu la kupokea na kushughulikia malalamiko ya wadau yanayohusu Ofisi ya Mkurugenzi wa
Manispaa.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa