MAJUKUMU YA HALMASHAURI YA MANISPAA YA MOROGORO
1. Kusimamia na kudumisha amani, ulinzi na usalama katika maeneo ya mipaka yake.
2. Kutengeneza mazingira mazuri kwa wawekezaji mfano STAR CITY, MJI MPYA WA KIEGEYA, KUJENGA MJI MKONGWE WA CHAMWINO N.K
3. Kuhamasisha/kuendeleza na kuwapatia huduma bora za kijamii na kiuchumi wananchi walio katika eneo la mipaka ya Halmashauri.
4. Kusimamia utekelezaji wa sera za maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika maeneo yao.
5. Kuchukua hatua madhubuti za kuendeleza na kuhifadhi mazingira.
6. Kusimamia Utawala,fedha mambo yote ya uendeshaji katika ngazi mbalimbali zilizo ndani ya mamlaka ya Halmashauri ya Manispaa.
7. Kusimamia na kuhakikisha demokrasia inadumishwa katika jamii.
8. Kukusanya mapato yatakayowezesha mamlaka ya serikali ya mtaa kuendesha shuguli zake pamoja na kutoa taarifa za matumizi kupitia kamati mbalimbali.
9. Kutoa huduma mbalimbali za kiuchumi na kijamii pamoja na kutekeleza shughuli za maendeleo katika maeneo yao.
10.Kuzingatia na kutambua masuala mtambuka kama vile jinsia.
11.Kuendeleza na kusimamia kanuni za biashara, viwanda na kilimo.
12. Kubuni mikakati ya kupambana na umaskini pamoja pamoja na mbinu za kusaidia kuboresha maisha ya vijana, wazee na walemavu
13.Kusimamia na kuendeleza huduma za afya, elimu, maji, utamaduni na masuala ya burudani katika jamii.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa