MKURUGENZI WA MANISPAA YA MOROGORO ANAWATANGAZIA WANANCHI WOTE WA MANISPAA YA MOROGORO KUWA HAIRUHUSIWI KUFANYA UJENZI WOWOTE NDANI YA MIPAKA YA HALMASHAURI YA MANISPAA YA MOROGORO BILA KUWA NA VIBALI VYA UJENZI , HII INAHUSISHA MAENEO YA MANISPAA ; YALIYOPIMWA NA AMBAYO HAYAJAPIMWA PAMOJA NA WENYE HATI MILIKI ZA ARDHI NA WASIO NAZO.
HII NI KWA MUJIBU WA SHERIA YA MIPANGO MIJI NA.8 YA MWAKA 2007 KIFUNGU KIDOGO CHA 1& 2 PIA KIFUNGU CHA 124 CHA KANUNI ZA SERIKALI ZA MITAA ZINAZOSIMAMIA UJENZI MJINI ZILIZOTANGAZWA KWENYE GAZETI LA SERIKALI Na.242 LA MWAKA 2008.
KWA TANGAZO HILI WANANCHI WOTE WALIOVUNJA SHERIA KWA KUFANYA UJENZI BILA VIBALI VYA UJENZI WANAPEWA MUDA WA SIKU 14 KUANZIA TAREHE 18/02/2020 KUFIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA MOROGORO KUOMBA VIBALI VYA UJENZI KWA HIARI , AMBAPO KATIKA KIPINDI HICHO CHA MSAMAHA HAKUTAKUWA NA FAINI.
BAADA YA MUDA ULIOTOLEWA KUISHA HALMASHAURI YA MANISPAA YA MOROGORO ITAENDESHA OPERESHENI MAALUM YA UKAGUZI KATIKA MAENEO YOTE YA MANISPAA NA WALE WATAKAOKUTWA HAWANA VIBALI VYA UJENZI WATALIPA FAINI AMBAYO NI 2% YA UJENZI /MAENDELEZO WALIYOFANYA , FAINI HII INATOZWA KWA MUJIBU WA SHERIA YA ARDHI YA MWAKA 1999.
AIDHA, KWA WALE WATAKAO KAIDI KUZINGATIA AGIZO HILI HATUA ZA KISHERIA ZITACHUKULIWA DHIDI YAO AMBAPO HALMASHAURI YA MANISPAA YA MOROGORO KWA MAMLAKA ILIYOPEWA CHINI YA KIFUNGU CHA 139 CHA SHERIA YA SERIKALI ZA MITAA (LOCAL GOVERNMENT (URBAN AUTHORITIES) ILIYOTANGAZWA KWENYE GAZETI LA SERIKALI NA.242 LA MWAKA 2008 ITAONDOSHA/ITABOMOA MAENDELEO YOTE IKIWA NA MAANA YA MISINGI, MABOMA,UZIO NA MAJENGO YOTE YALIYOJENGWA BILA VIBALI, AMBAPO WAMILIKI WAKE WATAWAJIBIKA KUREJESHA GHARAMA ZOTE ZITAKAZOTUMIWA NA HALMASHAURI YA MANISPAA YA MOROGORO KUBOMOA /KUONDOSHA MAENDELEO HAYO.
HILI NI TANGAZO LA MWISHO : ZINGATIENI AGIZO HILI ILI KUEPUKA USUMBUFU AU HASARA ZINAZOWEZA KUJITOKEZA.
TANGAZO HILI LIMETOLEWA NA
SHEILLA EDWARD LUKUBA
MKURUGENZI MANISPAA YA MOROGORO
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa