• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Morogoro Municipal Council
Morogoro Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
    • Wakuu wa Divisheni na Watumishi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Divisheni
      • Rasilimaliwatu na Utawala
      • Miundombinu, Uendelezaji wa Vijijini na Mijini
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ugavi na Manunuzi
      • Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Fedha na Uhasibu
      • Taka Ngumu na Usafishaji
      • Michezo, Sanaa na Utamaduni
      • TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Mazingira
    • Miundombinu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao Vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyoisha
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Fomu ya Maombi
    • Waraka
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
  • Market
    • Market line 1
    • Maket line 2

BARABARA ZA MAYELE, VETA, TUNGI NA TUBUYU KUWEKWA LAMI MWAKA HUU

Posted on: November 22nd, 2023

Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, ndugu Ally Machela ameuambia umma wa Manispaa hiyo kwamba barabara zenye urefu wa kilomita 20.5, katika Kata za Chamwino, Tungi, Tubuyu na Kihonda zinatazamiwa kujengwa kwa kiwango cha lami, kupitia mradi wa kuboresha miji wa TACTIC.

Mkurugenzi Machela ameyasema hayo alipokuwa akizungumzia hali ya barabara za Manispaa kwa sasa, alipokuwa katika kikao na waandishi wa habari wa kituo cha Redio na Televisheni cha Abood, ambapo ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuiteua Manispaa ya Morogoro kuwa miongoni mwa wanufaika wa mradi wa TACTIC katika awamu hii ya kwanza ya utekelezaji wake kwani hali ya barabara za Manispaa hiyo kwa sasa ni mbaya kwa sababu kuna mitaa haipitiki na iko mjini.

 “Kupitia mradi wa TACTIC barabara za lami zitakazojengwa ni barabara ya VETA Kihonda, barabara ya Tungi mpaka Star City, barabara ya Tubuyu mpaka Nanenane makaburini na barabara iliyobatizwa jina Mayele kutokana na mtetemeko wake pindi  vyombo vya usafiri vinapopita juu yake huko kwenye Kata ya Chamwino.

Vilevile kupitia TACTIC, mifereji yenye urefu wa kilomita 4.4 itajengwa, ukiwemo mfereji korofi huko Mazimbu, ambao mara nyingi katika vipindi vya mvua umekuwa kero kubwa kwa wananchi wa Kata hiyo. Na mara ujenzi wa barabara hizo na mifereji hiyo utakapokamilika, tutavikabidhi kwa TARURA kwa ajili ya usimamizi zaidi” alifafanua  Machela.

Kwa upande mwingine, Mkurugenzi Machela alibainisha jitiada za Manispaa katika kuisaidia TARURA kuhakikisha Manispaa inakuwa na barabara zinazopitika, ambapo alisema katika mwaka huu, Manispaa imefungua barabara zaidi ya kilomita 120 kwenye eneo la Kiegea Kata ya Mkundi, na kujenga vivuko kwenye Kata za pembezoni kama vile Kata ya Ruhungo na sasa Kata za Bigwa na Mindu ndizo zitakazofuatia kujengewa vivuko.

Aidha, Mkurugenzi Machela amesema, mwaka huu Manispaa imetenga zaidi ya shilingi milioni 700 kwa ajili ya kununua greda ambalo italikabidhi kwa TARURA ili kuchagiza kasi ya uchongaji wa barabara za pembezoni mwa Manispaa na kuhakikisha wananchi wa Manispaa ya Morogoro wanakuwa na barabara nzuri zinazopitika wakati wote.

MWISHO

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI February 19, 2025
  • FURSA YA UWEKEZAJI KWA NJIA YA UBIA(PPP) February 18, 2025
  • ZABUNI YA UPANGISHAJI ENEO LA ROCK GARDEN MANISPAA YA MOROGORO August 16, 2022
  • MAPOKEZI YA HELA ZA OC KWA MWEZI JULAI 2022 KIASI CHA TSH 8,714,000.00 August 10, 2022
  • Angalia Yote

Habari Mpya

  • BARAZA LA MADIWANI NA WATUMISHI MANISPAA YA MOROGORO WAFANYA ZIARA YA MAFUNZO HALMASHAURI YA JIJI TANGA

    April 26, 2025
  • KAMATI YA KUDHIBITI UKIMWI MANISPAA YA MOROGORO YATAKA KASI VITA DHIDI YA MAAMBUKIZI MAPYA.

    April 17, 2025
  • KAMATI YA HUDUMA ZA UCHUMI, AFYA NA ELIMU MANISPAA YA MOROGORO YARIDHISHWA NA KASI YA MIRADI YA MAENDELEO.

    April 15, 2025
  • MWENGE WA UHURU KITAIFA WAZINDUA MIRADI YA MAENDELEO YENYE THAMANI ZAIDI YA BILIONI 1.8.

    April 12, 2025
  • Angalia Yote

Video

MEYA KIHANGA AKABIDHI TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI ZAIDI YA 1600 WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Leseni za Biashara
  • Sheria Ndogo za Manispaa ya Morogoro
  • Sisi ni Nani

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Tamisemi
  • Morogoro Modern Market system (outside)
  • Tovuti ya Utumishi
  • Morogoro Modern Market System (LAN Network)
  • Tovuti Rasmi ya Ikulu
  • Tovuti ya RAS Morogoro

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro

    Anuani: 166 morogoro

    Simu: 0232614727

    Simu: 0734-039300

    Baruapepe : info@morogoromc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa