Ofisi ya Mashtaka ya mkoa wa Morogoro imewaonya baadhi yavijana wa Bodaboda kuachana na tabia ya kuwafuatilia na kuwarubuni wanafunzi wakike wa shule za msingi na sekondari kwani watajikuta wakifungwa miaka 30 nakuzeekea jela.
Mkuuwa Mshitaka mkoa wa Morogoro , Neema Haule alisema hayo kwenye hotubayake wakati wa maadhimisho ya siku ya huduma ya msaada wa kisheriangazi ya kimkoa iliyofanyika Oktoba 23, 2019 katikaviwanja vya Ofisi ya Mtendaji Kata ya Chamwino, Manispaaya Morogoro.
Pamojana tahadhari hiyo imesema pia, ipo hajaya kutolewa elimu kwa wananchi wa mkoa huo kuhusu sheriaza makosa mbalimbali yakiwemo ya ubakaji kwa vile, imebainika kuwavijana wanaojihusisha na boda boda kuanziaumri wa miaka 19 wamekuwa wakikutwa na hatia ya makosa yaubakaji wanafunzi wa kike na kufungwa miaka 30 jela.
Alisema,ni vyema ikatengwa siku muafaka ya kukaa na kuratibu migogoro ya wananchiinayojitokeza kwa kushirikiana kati ya timu ya uongozi wa halmashauri za wilaya, wadau na Ofisi ya mkuu wa wilaya.
Haulealisema ,wakati mwingine wananchi wanahitaji kujua sheria zinasemajena watu kuelimishwa aina mbalimbali ya makosa na adhabuzake yakiwemo ya makosa ya ubakaji watoto chini ya umri wa miaka 10pamoja na wanafunzi wa shule .
“Tunajukumu kubwa kazi ya mitaa , kitongoji , kijiji na kata ya kuelimishawananchi hasa bodaboda waache kuwafualiawanafunzi wakike…ninasema hivyo kwa sababu mimi ndiye ninayesomamashikata yote yanayokuja mezani kwangu “ alisema Haule na kuongeza.
“Nasikitika sana bodaboda ana miaka 19 , anakwenda kufungwa miaka 30 , akitokahuko anakuwa babu , hana mtoto, hana kitu chochote anakuwa ameshazeeka , tegemezihata nguvu za kuzaa tena hazipo, lazima niseme ukweli ” alisisitiza Haule.
Mkuuwa Mshitaka wa mkoa huyo alitumia fursa hiyo kuwatahadharisha Boda boda kuwawabadirike na kuacha tabia ya kuwafuatafuata wanafunzi wa shule nakuwaona ni hatari kwao.
‘Najua wengi mpo hapa leo ( jana ) na muelezane huko vijiweni wanafunzi wa kikeni hatari , unaenda kumchukua ameridhia mwenyewe , lakini chini ya miaka 18 ,sheria haiangalii hiyo ya kuridhia kwake , sheria inamtambua ni mtoto hivyo waogopwekama ukoma” alisema .
Pamojana hayo , alisikitishwa kuona watoto wanabakwa halafu wazazi hasaakina mama wanakwenda kuelewana na upande wapili na kumfanya mtoto asiende kutoa ushahidi.
“Mkoa wa Morogoro umekuwa ni waajabu sana , watoto wanabakwa , halafu mamaanakwenda kuelewana na upande wapili ‘ alisema na kuongeza.
“Haya mambo tumekuwa tukiyashuhudia , ni jambo la kusikitisha sana , tunaombaakina mama mbadirike , tumtendee haki mtoto yule ambaye kwa sasahana sauti kwa wakatu huu , lakini kesho na kesho kutwa ni nguvu yataifa“ alisema Haule.
Kwamujibu wa Mkuu wa Mshitaka wa mkoa kuwa , sheria inasema mtotoakibakwa akiwa chini ya umri wa miaka 10, mtuatakayekutwa na hatia hiyo anafungwa kifungo cha maisha jela.
Piaalitoa wito kwa kila kijiji, kata wilaya na mkoa kuimalisha kamati zakutokemeza ukatili kwa wanawake na watoto na hilo si kwa viongozi pekee bali nawananchi kwa ujumla wao.
Haule, pia alisikitishwana taarifa iliyoonesha kuwepo kwa idadi kubwa ya watuwaliojitokeza kuwasilisha malalamiko mbalimbali mbele yawatoa huduma na serikali na hilo linaonesha udhaifu kwa watendaji wangazi mbalimbali ndani ya mkoa ya utoaji wa haki kwa wananchi.
“Hii haikubaliki hata kidogo , lazima watoa huduma , wanasheria na wataalaamuwasimamie suala hili na wahakikishe wanajipanga ilib mkoa huu uwehuru kutokana na kero hizi’ alisema Haule .
NayeMratibu wa Maadhimisho hayo , Erasto Mfugale alisema ,kwa mwakammoja uliopita (2018) watu 4,534 kati ya hao wanawake 2,877 nawanaume 1,657 walijitokeaa kuwasilisha malalamiko yao mbalimbali mbele ya watoahuduma na serikali .
Mfugalealitaja kesi za ardhi ziliongoza kufikia 1,122 na kuchukua asilimia25 ya watu wote , migogoro ya ndoa 951 sawa na asilimia 21 , matunzoya watoto kesi 867 sawa na asilimia 19, mirathi404, madai 428, kesi za jinai 102, ukatili wa kijinsia watu 362, kesi za kazi 166 na kesi nyinginezo ni 132.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa