Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Bi Regina Chonjo amewaagiza wafanyabiashara(wamachinga) wote waliopanga bidhaa chini katikati ya mji kurudi katika masoko ndani ya siku saba kuanzia jana tarehe 19/06/2018.
Mkuu huyo wa Wilaya alizungumza hayo wakati wa ziara aliyofanya jana ya kukagua masoko yote yaliyopo ndani ya Manispaa ya Morogoro na kukuta vizimba na vioski vingi vikiwa wazi baada ya kuachwa na wafanyabiashara na wengi kukimbilia mjini kwa lengo la kufata wateja .Ziara hiyo ilihusisha soko la Nanenane,Mazimbu,Mawenzi Manzese na Mnada wa Kikundi.
Katika ziara hiyo soko la Nanenane liligundulika kuwa na vioski 202,vinavyotumika ni 10,vizimba 208 vinavyotumika ni 9, wakati soko la Mazimbu lina vizimba 380 na vinavyotumika ni 40 tu na vioski 161 ila vinavyofanya kazi ni 7 tu na katika soko Manzese kuna vizimba 1080 ila vinavyotumika ni 480 na vioski na soko la Mawenzi kuna jumla ya vizimba 883 ila vinavyotumika ni 852 na kuna jumla ya vioski 82 ila vinavyotumika ni 82.Aidha katika soko la Mawenzi ilielezwa kuwa baadhi ya wafanyabiashara wamehama na kuhamia mjini kati kwaajili ya kufanya biashara.
"Lengo lilikuwa ni kuwasidia wakina mama ambao wana mitaji midogo na wanaotembeza biashara zao katikati ya mji ila kilichotokea ni wafanyabiashara wamekuwa wakihama katika masoko na kuleta bidhaa katikati ya mji na kufanya soko katika maeneo ya barabara kuu,kitu ambacho ni hatari ata kwa wapita kwa miguu na magari".Alisema Mkuu uyo wa Wilaya.
Aidha ameuagiza uongozi wa Manispaa kufunga magenge bubu yote yaliyoanzishwa mitaani ili kufanya biashara za masoko ziweze kushamiri na wafanyabiashara kulipa kodi kwa wakati.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa