• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Morogoro Municipal Council
Morogoro Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
    • Wakuu wa Divisheni na Watumishi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Divisheni
      • Rasilimaliwatu na Utawala
      • Miundombinu, Uendelezaji wa Vijijini na Mijini
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ugavi na Manunuzi
      • Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Fedha na Uhasibu
      • Taka Ngumu na Usafishaji
      • Michezo, Sanaa na Utamaduni
      • TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Mazingira
    • Miundombinu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao Vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyoisha
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Fomu ya Maombi
    • Waraka
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
  • Market
    • Market line 1
    • Maket line 2

DC CHONJO AZINDUA WODI YA WAZAZI SABASABA, HUKU AKIWATAKA WAUGUZI KUTUMIA TAALUMA ZAO ILI WAZAZI WAJIFUNGUE SALAMA

Posted on: April 21st, 2020

MKUU wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Regina Chonjo , amezindua rasmi Wodi ya Wazazi ijulikanyo kwa jina la "Wodi ya Wazazi Regina Chonjo" katika Kituo cha Afya cha Sabasaba Manispaa ya Morogoro.

Akizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya uzinduzi huo, Chonjo, amewataka wauguzi kutumia taaluma zao kwa weledi ili wazazi wajifungue salama.

Aidha, amekipongeza kituo hicho cha afya kwani tangia kianze huduma ya uzalishaji haijawai kutokea kifo cha mzazi wala mtoto huku akisema jambo hilo linastahili pongezi kwani wauguzi wamekuwa makini na wanazingatia waledi kazini.

"Kituo kizuri sana, kwanza hongereni nimesikia taarifa ikisomwa kwamba tangia mtoe huduma hii ya kujifungua kwa Wazazi wetu, hakuna matukio ya vifo, endeleeni hivyo hivyo kuwahudumia wazazi vizuri, mimi sitegemei kupata malalamiko hadi Wazazi wakaanza kukimbilia Vituo vyingine, mmeonyesha mnaweza na sisi tunawategememea katika kutoa huduma bora na kuwafanya wakina mama kuja kwa wingi katika Kituo chetu kutokana na ubora wa huduma zinazopatikana hapa" Amesema Chonjo.

Amesema lengo la Serikali kujenga Jengo hilo la Wodi ya Wazazi ni kuwawezesha Wananchi (wakina mama wajawazito ) kupata huduma za kujifungulia karibu na makazi yao ili kupunguza vifo vya Mama  na mtoto pamoja na kuwapunguzia umbali wa kufuata huduma za afya Hospitali ya Mkoa.

DC Chonjo, amelishukuru sana Baraza la Madiwani linaloongozwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga, Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba pamoja na Watumishi wote wa Manispaa kwa kazi nzuri waliyoifanya kwa kuzingatia maelekezo na maagizo hadi wakaipa jina lake Wodi hiyo jambo ambalo limemfanya ajisikie furaha na limeendelea kumpa heshima kubwa na kuacha alama katika utawala wake katika upande wa afya.

"Nimekuwa nikitoa ushauri juu ya Jengo hili, nashukuru wamenielewa , Viongozi wa Manispaa wamekuwa waelewa sana, hata pale unapowakosoa wamekuwa wepesi kujirekebisha na kufanya kazi kwa weledi wa hali ya juu sana, hata kama ningekuwa na ushauri zaidi ya Malaika lakini kama Viongozi hawa wangekuwa wamevurugwa tusingefikia huku, nilipofika Manispaa hii mwaka 2016 nilikuta janga la ugonjwa wa Kipindupindu miaka 5 mfululizo , lakini tulijitahidi kushirikiana ndani ya miezi 3 ugonjwa huo ukabakia kuwa historia hii inaonyesha uongozi wa pamoja unavyotakiwa kuwepo , inafikia wakati naumia sana kuona pale mama mjamzito anajifungua na kupoteza maisha au kupoteza kichanga chake, hivyo tuliona umuhimu wa kuongeza jengo la wodi ya Wazazi bila kuwachanganya na Wagonjwa wengine na nimeridhishwa na ujenzi wake na jengo limeonyesha thamani ya pesa , nimpongeze Mkurugenzi wa Manispaa hii amenitendea haki hadi wanakubali kuipa jina langu hakika ni heshima kubwa wamenipatia ingewezekana wakaiita jina jengine lakini hawakufanya hivyo nawashukuru sana "Ameongeza DC Chonjo.


Katika hatua nyingine, DC Chonjo, amepongeza hatua zilizochukuliwa na Manispaa ya Morogoro kufuatia agizo lake la kutaka Manispaa hiyo kutengeneza vitakasa mikono kwa kutumia malighafi ya ndani kama alivyosisitiza Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
Amesema vitakasa mikono vitauzwa kwa bei elekezi ya Shilingi 2500/= kama alivyoelekeza ili kila mwananchi awe na uwezo wa kununua ukilinganisha bei ya dukani kuwa juu sana.

Hata hivyo, DC Chonjo , amechukizwa na baadhi ya wazazi kushindwa kuwafungia watoto wao ndani wakati Serikali ilishatoa mapumziko kwa Wanafunzi katika janga hili la CORONA.

Amesema jukumu la ulinzi wa Mtoto nyumbani ni la Wazazi/Walezi lakini bado watoto wanazurura hovyo , unaweza kuta baada ya kurudi shule wanafunzi hawa nusu yake wakawa Wazazi katika Wodi ya Regina Chonjo.

Pia DC Chonjo, amepiga marufuku na kuwaomba wakulima wa vyakula kuacha tamaa ya kuuza vyakula vyao vikiwa vichanga mashambani badala yake waviache ili kuweka akiba ya chakula kukwepa kukaribisha njaa siku za usoni.

Mwisho , DC Chonjo, ameuomba Uongozi wa Manispaa ikiwemo Baraza la Madiwani, pamoja na Ofisi ya Mkurugenzi kuona haja ya kuongeza Jengo la Chumba cha upasuaji ili kuendelea kuokoa maisha ya Wakina mama mara wanapopata shida kubwa kwani Hospitali ya Mkoa ipo mbali inaweza kupelekea kupoteza maisha ya wakina mama wakati wa kuwakimbiza hositali kubwa.

Naye Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro, amesema kuwa Manispaa imejitahidi kuimarisha Vituo vya afya hususani katika Wodi za Wazazi ili kuhakikisha mama wajawazito wanazaa kwa usalama bila kupoteza maisha.

Amesema kutokana na ombi la Mkuu wa Wilaya la kutaka kuongeza Jengo la Chumba cha upasuaji amelipokea na atalifikisha katika vikao vya Baraza ili katika mwaka wa fedha 2020/2021waweze kuliingiza katika bajeti.


Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Morogoro Mjini, Ndg. Fikiri Juma, ameipongeza Manispaa ya Morogoro kwa utekelezaji wa Miradi mingi iliyomalizika na inayoendelea kutekelezwa.
Amesema ameshuhudia Maboma ya Shule za Sekondari na Msingi yakimalizika , Vituo vya afya, Ofisi za Watendaji hii imetokana na Manispaa kutekeleza vyema na kwa viwango vya kisasa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM ).

"Kikubwa zaidi ,, nimefurahishwa na jina la Wodi hii, kiukweli Manispaa mmemtendea haki Mama yetu Regina Chonjo, amekuwa mstari wa mbele sana katika kuchochea maendeleo katika Wilaya yetu, tangia tuwe naye mwaka 2016 yapo mengi mazuri yamefanyika na tumeona uongozi wake uliotukuka, ningeshangaa sana jina lake lingekuwa katika Jengo baya, yeye ni DC wa Viwango na Jengo pia lina viwango "Amesema Fikiri.

Kwa upande wa Afisa Muuguzi wa Kituo cha afya Sabasaba, Dr. Vulfrida Kyara, amesema jengo hilo lilifunguliwa Agosti ,2019 likiwa na uwezo wa kuhudumia wakina mama 18 kwa wakati mmoja huku lengo likiwa ni kuwahudumia wakinana wapatao 2585 wa Kata ya sabasaba lakini mpaka sasa ina hudumia zaidi ya hao huku wengine wakiwa wanatokea Kata mbalimbali za Manispaa na nje ya Manispaa.

Amesema mpaka sasa wakina mama waliolazwa katika wodi hiyo wamefikia 965, ambapo kati ya hao waliojifungulia Kituoni hapo ni wakina mama 714 sawa na asilimia 74% na wakina mama 251 sawa na asilimia 26% walipewa rufaa kwenda Hospitali ya Mkoa kwa ajili ya huduma kama ya upasuaji ambayo haipatikani kituoni hapo.

Aidha, amesema pamoja na mafanikio makubwa yaliyopatikana katika utoaji huduma , zipo changamoto ikiwemo kukosekana kwa chumba cha upasuaji hali inayosababisha rufaa nyingi zisizo za lazima, ukosefu wa chumba maalum na vifaa kwa ajili ya watoto pamoja na ukosefu wa Jenereta kubwa lenye uwezo wa kukidhi mahitaji hivyo kupelekea ugumu wa huduma pale umeme unapokatika.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI February 19, 2025
  • FURSA YA UWEKEZAJI KWA NJIA YA UBIA(PPP) February 18, 2025
  • ZABUNI YA UPANGISHAJI ENEO LA ROCK GARDEN MANISPAA YA MOROGORO August 16, 2022
  • MAPOKEZI YA HELA ZA OC KWA MWEZI JULAI 2022 KIASI CHA TSH 8,714,000.00 August 10, 2022
  • Angalia Yote

Habari Mpya

  • BARAZA LA MADIWANI NA WATUMISHI MANISPAA YA MOROGORO WAFANYA ZIARA YA MAFUNZO HALMASHAURI YA JIJI TANGA

    April 26, 2025
  • KAMATI YA KUDHIBITI UKIMWI MANISPAA YA MOROGORO YATAKA KASI VITA DHIDI YA MAAMBUKIZI MAPYA.

    April 17, 2025
  • KAMATI YA HUDUMA ZA UCHUMI, AFYA NA ELIMU MANISPAA YA MOROGORO YARIDHISHWA NA KASI YA MIRADI YA MAENDELEO.

    April 15, 2025
  • MWENGE WA UHURU KITAIFA WAZINDUA MIRADI YA MAENDELEO YENYE THAMANI ZAIDI YA BILIONI 1.8.

    April 12, 2025
  • Angalia Yote

Video

MEYA KIHANGA AKABIDHI TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI ZAIDI YA 1600 WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Leseni za Biashara
  • Sheria Ndogo za Manispaa ya Morogoro
  • Sisi ni Nani

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Tamisemi
  • Morogoro Modern Market system (outside)
  • Tovuti ya Utumishi
  • Morogoro Modern Market System (LAN Network)
  • Tovuti Rasmi ya Ikulu
  • Tovuti ya RAS Morogoro

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro

    Anuani: 166 morogoro

    Simu: 0232614727

    Simu: 0734-039300

    Baruapepe : info@morogoromc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa