MKUU wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Mussa Kilakala, amekabidhi Viti mwendo (Wheelchair) kwa watu wenye ulemavu Manispaa ya Morogoro.
Zoezi la ugawaji wa Viti mwendo limefanyika Ukumbi wa JKT Bwalo Desemba 11-2024 ambapo zaidi ya walemavu 30 wamepatiwa huduma hiyo ya viti mwendo.
DC Kilakala, amesema Serikali itaendelea kuwapa kipaumbele watu wenye ulemavu na kuhakikisha wanapata huduma bora zinazowahusu bila changamoto yoyote.
" Hii ni kumuunga mkono Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuwapa kipaumbele watu wenye ulemavu ambapo tumeshuhudia katika Serikali yake akiteua watu wenye ulemavu kushika nafasi mbalimbali," Amesema DC Kilakala.
Kwa upande wa Afisa Ustawi Manispaa ya Morogoro, Sidina Mathias ,amemshukuru Mkuu wa Wilaya huku akiahidi kuendelea kutoa ushirikiano mkubwa kwa watu wenye uhitaji maalum.
Naye miongoni mwa wazazi mwenye mtoto mlemavu, Eliusta Tembe,amemshukuru DC Kilakala kwa msaada wa viti hivyo huku akiziomba Taasisi zingine mbalimbali zijaribu kuwajali watu wenye ulemavu kwani wamekuwa na uhitaji mkubwa kila siku kwa maana kuna ongezeko kubwa la watu wenye ulemavu.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa