MKUU wa wilaya ya Morogoro,Regina Chonjo ametoa siku saba kufungasha virago watu wanaojishughulisha kuvyatua na kuchoma matofari kando ya barabara na daraja la mto Morogoro katika barabara ya mei mosi iliyojengwa kwa kiwango cha lami nzito ili kulinda hifadhi ya mazingira kwa mujibu wa sheria.
Barabara ya hiyo ni kisasa iliyokamilishwa kujengwa mwaka mmoja uliopita ina urefu wa kilometa 5.1 na iligharimu kiasi cha Sh 11,805,176,469.00 ambayo ni fedha za mkopo kutoka Benki ya Dunia.
Mkuu wa wilaya alitoa muda wa siku hizo Augost 28, 2018 kwa nyakati tofauti akiwa kwenye mkutano na wananchi uliofanyika Ofisi ya Kata ya Kichangani pamoja na wahusika wa ufyatuaji na uchomaji wa matofari kando ya barabara hiyo eneo la kata ya Kichangani.
Chonjo alifanya ziara ya ukaguzi wa miradi ya ujenzi wa barabara mpya za kiwango cha lami nzito ya Tubuyu, Nane Nane , Maelewano zenye jumla ya urefu wa kilometa 4.6 pamoja na kipande cha barabara cha urefu wa mita 275 kilichonjengwa ili kuunganisha na barabara hizo ambazo zilitengewa kiasi cha Sh 12,630,868,635 .
Alisema ,wapo watu wachache wanaojishughulisha na uchomaji wa matofari na wamechimba udongo hadi kando kando ya barabara na kwenye daraja na kuhatarisha uhai wa daraja hilo ikiwa na kuacha mashimo jambo ambalo halikubaliki kamwe.
“ Wale wanaochoma matofari wameendelea kusogea kuchimba udongo hadi kwenye kingo za barabara na daraja , likivunjika daraja hili ni adha kubwa kwa watu wengi wanatumia barabara hii “ alisema Chonjo .
Alisema ,imejengeka tabia kutoka kwa baadhi ya wananchi ya kuharibu miundombinu ya barabara baada ya miradi kukabidhiwa kwa halmashauri ikiwemo na kuchimbua kokoto zilizopo mpembezoni na kung’oa taa za barabarani kitendo kinacho hatarisha uhai na usalama wa miundombinu kwa manufaa ya jamii.
“ Hawa wanaochoma matofari nawapa siku saba waondoe matofari yao na wafukie mashimo yaliyosogerea barabara na daraja na Ofisa Mazingira wa Manispaa simamia zoezi hili waongoze waondoe tofari na kufukia mashimo .
Chonjo alisema ,barabara hizo zimejengwa kwa kutumia fedha nyingi za serikali ,hivyo ni wajibu wa wananchi wanaopitiwa nazo kuzitunza na kuwa walinzi wa kuwafichua wanaohujumu miundombinu ili waweze kushughulikiwa na vyombo vya dola.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa