MKUU wa Wilaya ya Morogoro, Mhe Regina Chonjo, anatarajia kufanya ziara ya kusikiliza na kutatua kero za Wananchi Novemba 7, 2019 kwenye viwanja vya hospitali ya rufaa morogoro kuanzia saa 4:00 Asubuhi.
Akizungumza leo Ofisini kwake, amesema lengo la ziara hiyo ni kusikiliza na kutatua kero za Wananchi ili kurahisisha huduma kwa jamii pamoja na kufahamu kuhusu miradi mbali mbali inayotekelezwa na kero zilizotatuliwa katika utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM chini ya Rais wa awamu ya tano, Mhe Dkt John Pombe Magufuli.
Aidha, amesema sio Wananchi wote wanauwezo wa kufika Ofisini kwake, hivyo utaratibu huo ameuweka ili kuwepo na chachu ya uwajibikaji.
"Ziara yangu ni ya kiutendaji, tumeona tuanze kushuka chini kuanzia huku ndio kuna changamoto nyingi, kwahiyo niwaombe Wananchi na wakazi wote Manispaa ya Morogoro njooni muulize maswali pamoja na kutoa kero zenu ili zishughulikiwe, tutakuwa na wakuu wa idara mbali mbali fika bila kukosa , tukifanya hivyo tunaamini tunaenda kupunguza kero katika Wilaya yetu" Amesema DC Chonjo.
Hata hivyo , amesema anatambua kero kubwa zaidi ni changamoto zilizopo katika ardhi, katika kulifanikisha hilo na kuona changamoto za ardhi zinafanyiwa kazi na kutatuliwa ataambatana na Jopo la Wanasheria ili kuwasikiliza Wananchi na kuwahudumia katika upande huo.
Miongoni mwa taasisi atakazo ambatana nazo ni TAKUKURU, UHAMIAJI, ARDHI, TRA,MORUWASA,TANESCO,PSSSF,SHIRIKA LA BIMA YA AFYA,NIDA,TARURA,WAWAKILISHI WA BENKI zote zinazotoa huduma ndani ya Manispaa ya Morogoro.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa