Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Albert Msando, amewaomba wadau mbalimbali wa maendeo kuendelea kuishauri Serikali katika kufanikisha miradi ya Maendeleo.
Hayo ameyasema , Oktoba 06/2021 katika Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Wilaya ya Morogoro (DCC) kilichofanyika Katika Ukumbi wa Mikutano wa Kilakala Soko Kuu la Chifu Kingalu Morogoro .
Akizungumza wakati wa kuongoza kikao hicho, DC Msando, ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya ushauri (DCC) amewataka wadau pamoja na wajumbe wote wa kamati ya Ushauri Wilaya kuendelea kuishauri serikali namna gani ya kuboresha utendaji wa kazi na kuleta maendeleo.
"Ninawaomba wajumbe wote wa kamati hii kuishauri serikali bila kuogopa kwani ushauri wenu ni tija kwa maendeleo ya wilaya yetu" Amesema Msando.
DC Msando, amesema kuwa lengo la kamati ya ushauri Wilaya ni kuhakikisha Wilaya na Halmashauri zinasonga mbele, hivyo wajumbe wasichoke na wawe huru kutoa mapendekezo yao kwa kuchangia mambo mbali mbali kwa mustakabali wa maendeleo ya Wilaya.
"Lengo la kamati ya ushauri ni kuishauri serikali , sisi tupo tukiwa Viongozi wa Wilaya tukisimamia Maendeleo, ili kuhakikisha Wilaya yetu na Halmashauri zetu zinasonga mbele kimaendeleo, siyo kwamba yote tunayoyafanya ni sahihi, na ndio maana lengo la kikao ni kutushauri namna gani ya kuboresha utendaji wetu ili kuleta maendeleo makubwa katika Wilaya na Halmashauri zetu " Amesema DC Msando.
Naye aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mstaafu , Mzee . Steven Mashishanga, ameipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kwa kusimamia vyema mapendekezo ya kamati ya ushauri.
" Wajumbe wanafanya kazi nzuri sana, lakini ni vyema katika vikao vijavyo vya kamati kila idara ikaonesha takwimu halisi katika taarifa zake zikiwamo changamoto , idadi ya upungufu wa watumishi ili kamati iweze kutoa ushauri" Amesema Mzee Mashishanga.
Kwa upande wa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoroo, Mhe. Pascal Kihanga, amewataka Wajumbe wa kamati ya ushauri kuzungumzia changamoto na kutoa ushauri kwa uhuru ili yatokanayo yaweze kufanyiwa kazi.
"Pongezi kwa watendaji wote kwa kushirikiana kwa pamoja, hayo yote tunayoyafanya ni kutokana na ushauri wenu, na leo pia Ushauri wenu tumeupokea na tutaufanyia kazi kama tunavyochukua siku zingine, Na kama mnaona jambo haliendi sawa ni ruksa kwenu kutoa ushauri kwa uhuru kabisa na sisi tutaupokea" Mhe, Kihanga.
Naye Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini, Mhe. Abdulazizi Abood, amesema atahakikisha kwamba yale maendeleo yanayotakiwa kufanywa yatafanyika kwa kuongeza msukumo Bungeni katika kuona miradi yote ambayo iempendekezwa inapitishwa.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro, Dr. Christine Ishengoma, amesema katika kufikia malengo lazima kuwe na maoni ya watu mbalimbali .
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa