MKUU wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Bakari Msulwa, amefufua matumani ya Mkazi wa Mtaa wa Shule Kata ya Kingolwira Manispaa ya Morogoro, Bi. Joyce Macha , baada ya kuagiza Shirika la Umeme TANESCO kumunganishia Umeme mkazi huyo.
Hayo yamejiri leo Julai 18,2020, wakati wa ziara yake ya kikazi ya kutatua kero za wananchi ambapo ameagiza Shirika la Umeme TANESCO Manispaa ya Morogoro kufikia kesho Julai 19,2020 kazi ya kuanza kuunganisha huduma ya umeme kwa mkazi huyo iwe imeshaanza.
Kauli hiyo ameitoa kufuatia mgogoro uliodumu kwa takribani miaka 5 tangia mwaka 2014 kati ya Bi. Joyce Macha na mmiliki wa Shule ya Sekondari Iyula Malaika iliyopo Kata ya Kingolwira ambaye aliendelea kushikiria msimamo wake wa kukataa mwananchi huyo kuwekewa huduma ya umeme kwa kile alichodai kwamba mkazi huyo alivamia katika eneo lake la Shule.
“Haiwezekani mtu akanyimwa huduma ya umeme, kila raia ana haki za kupata huduma bila kuvunja sheria za nchi, umeme uwekwe kwa mwananchi yeyote anaehitaji na mwenye uwezo wa kulipia gharama za kuunganisha hata kama nyumba yake ni ya udongo na kuezekwa kwa nyasi, lakini cha kusikitisha hata kama eneo hilo lingekuwa na kesi kubwa kiasi gani lazima mtu apate huduma kama haki yake ya msingi , kesi hii imeshamalizika , Kamishina ardhi alishatoa hukumu , na eneo hilo limebaki mali ya kimila na hakuna mwenye eneo hivyo mama huyu anatakiwa apate huduma haraka iwezekanvyo ili maisha yake yaende na maisha ya utoaji wa elimu yaende bila kuathiri shughuli za mtu yeyote” Amesema DC Msulwa.
Kwa upande wa Katibu Tawala Wilaya ya Morogoro, Bi. Ruth John, amempongeza Mkuu wa Wilaya kwa kulivalia njuga swala hilo na hatimaye haki imepatikana.
“Huu ni mgogoro wa muda mrefu, umekuwa ukitusumbua sana , lakini Mkuu wetu wa Wilaya amefika hapa amejionea lakini tunampongeza sana kwa vile ametoa maelekezo mazuri kutokana na hukumu ya Kamishina wa ardhi alivyoitoa, kikubwa familia hizi ziishi vizuri kwani wao bado ni majirani wanatakiwa washirikiane badala ya kuleteana chuki” Amesema DAS Ruth.
Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro , Sheilla Lukuba, amemuagiza Afisa ardhi wa Manispaa ya morogoro kuandaa michoro ya hapo ili wale wenye maeneo waweze kuyamiliki kihalali kufuatia maeneo hayo michoro yao kufutwa.
Afisa Ardhi Manispaa ya Morogoro, Gisbert Msemwa, amesema muda wowote wataanza utaratibu wa kuandaa michoro mipya ili maeneno hayo yaweze kupimwa na wenye maeneo waweze kuwa na hati miliki ya ardhi kwani mpaka sasa maeneo hayo ni ya kimila na hakuna mwenye umiliki wa ardhi.
“Hii kesi ya muda mrefu, lakini eleo imepatiwa ufumbuzi, sisi kazi yetu kuanda michoro na kama wenye maeneo watapenda tuendelee nao kupima tutayapima au wanaweza kuwapata watu wengine lakini kubwa zaidi hata eneno hili halikuwa limekusudiwa kuwa Shule bali eneo hili lilikuwa shamba hivyo hakuna taarifa ya kubadili matumizi ya eneo hili tuliyonayo, kwahiyo kuyapima na kuweka michoro kutampa fursa mmiliki wa Shule hii kubadilisha matumizi ya ardhi na kupata kibali rasmi cha ubadilishaji wa matumizi ya ardhi kutoka shamba kuja eneo a huduma ya shule””Amesema Msemwa.
Mkazi wa eneo hilo la Shule, Bi Joyce Macha, amemhukuru Mkuu wa Wilaya , Katibu Tawala, Mkurugenzi Manispaa ya Morogoro pamoja na Idara ya ardhi kwa kulipambania suala lake na hatimaye kuipata haki yake aliyokuwa akiisubiria kwa muda mrefu.
Amesema sasa ameanza kupata matumaini mapya ya kupata hudma ya umeme kwa muda mraefu na ameahidi kuendelea kushirikiana na majirani zake waliopo katika eneno hilo la shule kwani bado maisha yanaendelea.
Katika hatua nyingine DC Msulwa, , ameuomba Uongozi wa Machinga Manispaa ya Morogoro kufanya kazi kwa uwaledi katika kuwaongoza wamachinga ili waweze kujipanga vizuri na kufanya biashara zao katika maeneo yaliyo salama.
"Nimesikia hapa kuna watu wanajiita wazawa na wandewa, wanawatoza watu pesa kuwakodishia maeneo , tabia hiyo ife mara moja, mtu akiwa na kitambulisho cha Wajasiriamali haruhusiwi kutozwa hela, sasa chukueni hizo hela za wandewa ipo siku mtachukua hela za wandewa wenzenu bila kujijua na mtaangukia mahala pabaya,ridhikeni na vipato vyenu pesa hizi mnazochukua za moto " Ameongeza DC Msulwa.
Pia ameagiza kuanzia mnada ujao wafanyabiashara wote wanaofanya baishara katika maeneo ya Shule ya Msingi Kikundi, Ofisi ya Kata ya Sultan Area pamoja na Kituo cha Polisi Kikundi kuondoka maeneo hayo na wafanye biashara eneo ambalo wamepangiwa na kamati yake ya kuandaa maeneo inayoongozwa na Afisa Tarafa Manispaa ya Morogoro, Wenyeviti wa Mitaa pamoja na Uongozi wa Wamachinga Manispaa ya Morogoro.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa