• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Morogoro Municipal Council
Morogoro Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
    • Wakuu wa Divisheni na Watumishi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Divisheni
      • Rasilimaliwatu na Utawala
      • Miundombinu, Uendelezaji wa Vijijini na Mijini
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ugavi na Manunuzi
      • Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Fedha na Uhasibu
      • Taka Ngumu na Usafishaji
      • Michezo, Sanaa na Utamaduni
      • TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Mazingira
    • Miundombinu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao Vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyoisha
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Fomu ya Maombi
    • Waraka
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
  • Market
    • Market line 1
    • Maket line 2

DC MSULWA ATAKA MAONESHO YA NANE NANE YAWASAIDIE WAKULIMA NA WAFUGAJI ILI KUONGEZA TIJA KATIKA SHUGHULI ZA UZALISHAJI

Posted on: July 7th, 2020

MKUU wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Bakari Msulwa, ameziomba Halmashauri zote mbili Morogoro Vijijini pamoja na Manispaa ya Morogoro kuhakikisha Maonesho ya Kilimo na Mifugo (Nane Nane) katika Wilaya ya Morogoro yanawasaidia wakulima, wafugaji na wavuvi kwa kiasi kikubwa ili kuwawezesha kubadili shughuli zao na kuzifanya kuwa na tija inayoridhisha.

Hayo ameyazungumza leo Julai 07, 2020, wakati wa ziara ya kukagua na kutembelea vipando vya Shamba darasa la Manispaa ya Morogoro pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro ikiwa ni kuangalia namna ya maandalizi yanavyoendelea katika kuelekea katika maadhimisho hayo ya Kanda ya Mashariki yanayotarajiwa kuanza Agosti 1-8,2020 Mkoani Morogoro.


Akizungumza na waandishi wa habari, DC Msulwa, amesema Maonesho ya Nane Nane yamekuwepo kwa miaka mingi maeneo mbalimbali ya nchi katika Kanda mbalimbali na ukiyatembelea utakutana na vitu vya kuvutia sana hususani Teknolojia na mbinu bora za uzalishaji kilimo na mifugo ambazo zinauwezo wa kuleta tija kubwa lakini bado changamoto kubwa mambo yote bora na mazuri yanayopatikana kwenye Maonesho bado hayajaweza kumfikia mkulima kwenye ngazi za msingi.

Amesema , kuwa unaweza kwenda maeneo ya wakulima wenyewe ukashangaa kukuta mkulima analima kilimo cha kienyeji ambacho hakina manufaa.

 “Teknolojia inayooneshwa kwenye Maonesho haya bado haijaweza kuwafikia wakulima na wafugaji wetu kwenye vijiji vyao wanapoendeshea shughuli zao za kilimo na mifugo, lakini teknolojia na ubunifu unaopatikana kwenye Maonesho haya unahitaji kuwafikia wakulima wa chini kabisa, maana tusijekuwa tunaandaa maonehso haya kwa ajili ya tabaka la watu wenye nacho tukawasahau wale wa hali ya chini ambao ndio wanaojihusisha na kilimo na kuendesha maisha yao" Amesema DC Msulwa .

 Aidha, ametoa wito kwa Mamlaka zinazohusika kuhakikisha Mashamba darasa yote ya halmashauri zote mbili vinakuwa vituo vya kudumu na wakati wote wataalamu wa kilimo na mifugo wawepo kituoni hapo kipindi chote cha mwaka wakisimamia shughuli za kilimo na mifugo kituoni hapo na Halmashauri zote zilete Wakulima na Wafugaji wao kujifunza na kupata suluhisho la changamoto zinazowakabili katika shughuli zao za uzalishaji .

Hata hivyo, ameziagiza Halmashauri zote mbili ,kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wanaounga mkono shughuli za kilimo, mifugo na uvuvi waone namna wanavyoweza kuifikisha kwa wakulima na wafugaji wetu elimu inayopatikana kwenye Shamba darasa .

Mwisho, amewaomba wananchi ndani ya Wilaya ya Morogoro na nje ya Wilaya hususani wakulima, wafugaji na wavuvi kutembelea Maonesho hayo kwa wingi katika Shamba darasa ya Wilaya ya ,Morogoro kwa kuwa mambo mazuri yakujifunza yapo mengi kubwa likiwa jinsi Teknolojia na mbinu bora za kuongeza tija ya uzalishaji mazao ya kilimo na mifugo.

Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba, amewataka waangalizi wa Shamba darasa kutumia muda ulipo kukimbiza na na maandalizi ili waweze kufanya vizuri katika ngazi ya Kanda ya Mashariki.

“Niwaombe Maafisa Mifugo na Kilimo ngazi zote waongeze nguvu na waangalie maeneo haya kwa jicho la tatu, muda sio rafiki sana , tuna wiki 3 za maandalizi, tuhakikishe kila kinachotakiwa kimefanyika , Maonesho haya yapo ndani ya Manispa yetu na Wilaya yetu hatuna sababu za kufeli, naamni tukishirkiana kitimu na tukaongeza ubunifu tutashinda vigezo vyote vipo ndani ya uwezo wetu”Amesema Lukuba.

Kwa upande wa Afisa Kilimo Manispaa ya Morogoro, Michael Waluse, amesema maandalizi yanaendelea vizuri ambapo washiriki wakuu ni pamoja na wakulima, wawakilishi wa wakala wa makapuni ya pembejeo, wawakilishi wa wasindikaji wa mazo mbalimbali, wawakilishi wa kampuni za umwagiliaji, wawakilishi wa kampuni za dhana za kilimo pamoja na Idara mbalimbali za Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.

Aidha, amesema miongoni mwa bidhaa zitakadhooneshwa ndani ya banda ni pamoja na mazao mbalimbali yanayozalishwa na wakulima, bidhaa mbalimbali zinazosindikwa na wakulima na wadau, shughuli za vyama vya Ushirika, shughuli za mawakala wa kampuni za pembejeo, shughuli mbalimbali za Idara za Halamshauri, shughuli mbalimbali za vikundi vya Vijana na Wakina mama, shughuli za kongano la nguo na shughuli za wazalishaji wa miche ya maua na matunda.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI February 19, 2025
  • FURSA YA UWEKEZAJI KWA NJIA YA UBIA(PPP) February 18, 2025
  • ZABUNI YA UPANGISHAJI ENEO LA ROCK GARDEN MANISPAA YA MOROGORO August 16, 2022
  • MAPOKEZI YA HELA ZA OC KWA MWEZI JULAI 2022 KIASI CHA TSH 8,714,000.00 August 10, 2022
  • Angalia Yote

Habari Mpya

  • BARAZA LA MADIWANI NA WATUMISHI MANISPAA YA MOROGORO WAFANYA ZIARA YA MAFUNZO HALMASHAURI YA JIJI TANGA

    April 26, 2025
  • KAMATI YA KUDHIBITI UKIMWI MANISPAA YA MOROGORO YATAKA KASI VITA DHIDI YA MAAMBUKIZI MAPYA.

    April 17, 2025
  • KAMATI YA HUDUMA ZA UCHUMI, AFYA NA ELIMU MANISPAA YA MOROGORO YARIDHISHWA NA KASI YA MIRADI YA MAENDELEO.

    April 15, 2025
  • MWENGE WA UHURU KITAIFA WAZINDUA MIRADI YA MAENDELEO YENYE THAMANI ZAIDI YA BILIONI 1.8.

    April 12, 2025
  • Angalia Yote

Video

MEYA KIHANGA AKABIDHI TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI ZAIDI YA 1600 WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Leseni za Biashara
  • Sheria Ndogo za Manispaa ya Morogoro
  • Sisi ni Nani

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Tamisemi
  • Morogoro Modern Market system (outside)
  • Tovuti ya Utumishi
  • Morogoro Modern Market System (LAN Network)
  • Tovuti Rasmi ya Ikulu
  • Tovuti ya RAS Morogoro

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro

    Anuani: 166 morogoro

    Simu: 0232614727

    Simu: 0734-039300

    Baruapepe : info@morogoromc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa