Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mheshimiwa Rebecca Nsemwa, amezindua Kliniki ya Ardhi, Manispaa ya Morogoro ikiwa na lengo la kuhakikisha migogoro ya ardhi inatatuliwa.
Uzinduzi huo umefanyika tarehe 23.10.2023 katika Ofisi ya ardhi, ya Manispaa, iliyopo Stendi ya Daladala Mafiga na kuhudhuriwa na mamia ya wananchi.
“Kliniki yetu ya ardhi ina lengo la kuhakikisha wananchi wa Manispaa ya Morogoro hawalii kwa sababu ya Ardhi. Haya ni maelekezo ya Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan ndio maana tumezindua Kliniki hii ili kushughulikia migogoro ya wananchi” amesema DC Nsemwa.
Kwa upande wake Kamishina Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Morogoro, ndugu Frank Minzkunte, amesema ili kurahisisha zoezi la upimaji na utoaji wa hati za viwanja, ni muhimu wananchi kuepuka migogoro ya ardhi, huku akisisitiza suala la Wananchi kuzingatia matumizi sahihi ya ardhi kwa kutokufanya kitu chochote kwenye ardhi kinachoweza kuwa kero kwa wengine.
Naye Msimamizi wa Sekta ya Ardhi Manispaa ya Morogoro, Bi. Emiline Kihunrwa, amesema zipo faida za umiliki ikiwemo dhamana ya mali isiyo hamishika kwenye baadhi ya mahitaji ya kisheria.
Kliniki ya Ardhi imewaweka pamoja wataalam wote wa sekta ya Ardhi wa Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Morogoro na wa Manispaa ya Morogoro ili kupokea, kusikiliza na kutatua migogoro ya ardhi ya wananchi wa Manispaa ya Morogoro.
MWISHO
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa