Wananchi wanao nufaika na mpango wa kunusuru kaya masikini Manispaa ya Morogoro,wametakiwa kuhakikisha wanatumia fedha wanazopata kukata bima ya afya pamoja na kugawa katika matumizi mengine muhimu na ya msingi ili kuweza kujikwamua kiuchumi.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Regina Chonjo wakati alipokuwa akitembelea kaya hizo ili kuhakikisha ikiwa fedha zinazo tolewa na TASAF zinawafikia walengwa kwa wakati na kutumika katika matumizi sahihi.
Amesema kuwa Mratibu wa TASAF wilaya anapaswa kuhamasisha zoezi la kila kaya kukata bima ya afya ili kuweza kusaidia gharama za matibabu kwa kaya hizo,kwani suala la matibabu limekuwa changamoto kwa walio wengi kushindwa kumudu fedha za matibabu kutokana na kukosa bima ya afya.
Chonjo ameongeza kuwa kila kaya inayo nufaika na ruzuku hiyo kutoka TASAF zinapaswa kubuni miradi midogomidogo kama vile ufugaji wa kuku,mbuzi, kondoo na bustani za mbogamboga ili kuweza kuzalisha mali itakayo wasaidia kutatua matatizo yao ikiwa mpango huo utafikia tamati,jambo litakalo kuwa lime wajengea uwezo wa kujitegemea.
Aidha Chonjo amewasisitiza wakazi hao kwa walioamua kujiendeleza kibiashara kuhakikisha wananunua vitambulisho vya wajasiriamali vilivyotolewana na Mhe.Dkt John P.Magufuli Rais wa Jamhuri ya Tanzania ili wasiweze kupata usumbufu wakati wakifanya biashara zao wawapo mitaani.
Naye Bi Consolata Hermani ambaye ni mnufaika wa Mpango wa kunusuru kaya maskini TASAFametoa shukrani kwa Mhe.Rais Dkt J.Magufuli kwa kuendelea kuwajari wananchi wenye uwezo mdogo na kumuomba aendelee kuwasaidia ili wawezee kujikwamua kiuchumi.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa