Serikali ya awamu ya tano inayodhamira ya dhati kwa kuhakikisha wananchi wake wanakuwa na maisha bora ikiwa na pamoja ni kuwezesha kujiletea maendeleo yao kupitia Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA).
Mratibu wa Mpango huo nchini , Seraphia Mgembe alisema hayo juzi ( Augost 20, 2018) wakati wa ziara na ujumbe wake alipozungumza na wakazi wa Kata ya Kihonda , Manispaa ya Morogoro.
Alisema ,dhamira ya serikali kupitia MKURABITA ni kuwaletea neema wakazi wa Manispaa ya Morogoro kupitia viongozi wake kushirikiana na wa mpango huo kwa kufanikisha upimaji wa viwanja 1,080.
“ Ni dhamira ya Serikali kutaka wananchi kuwa na maisha bora na kuwezesha kujiletea maendeleo kupitia mpango huu wa urasimishji” alisema Mgembe.
Alisema , wananchi walionufaika na urasimishaji wa ardhi kupitia mpango huo wanazo fursa za kuzitumia hati za umiliki wa ardhi kwa kujiletea maendeleo ikiwemo kujipatia mikopo kutoka taasisi za fedha.
Hata hivyo aliwasihi wananchi ambao walishapimiwa maeneo yao kupitia mpango huo kuchukua hati zao katika Mamlaka husika ili wazitumie katika kuchochea maendeleo miongoni mwao.
Mgembe alisema , Serikali kwa kuona umuhimu wa kuwawezesha wananchi imeanzisha dirisha moja la huduma kwa wananchi katika ofisi za Manispaa ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za uwezeshaji kwa wananchi ili waondokane na umasikini.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Urasimishji Rasilimali Ardhi na Biashara, Japhet Werema alisema kuwa, Mpango huo unazijengea uwezo halmashuri ili ziweze kushiriki katika urasimishaji wa Ardhi mijini na vijijini.
Kwa upande wake , Mpima Ardhi wa Halmashuri ya Manispaa ya Morogoro , Saimon Seja alisema kuwa hadi sasa jumla ya viwanja 558 katika mtaa wa Tuelewane vimekwishapimwa, 264 Mtaa wa Kihonda “B” na Folcal Land viwanja 258 na hivyo kufanya jumla ya viwanja vyote kufikia 1,080.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa