Wanafunzi wa kike wa Shule ya Sekondari Mbuyuni Modern, Manispaa ya Morogoro, wametakiwa kujitambua na kufahamu wajibu wao kwa jamii inayowazunguka huku wakijiepusha na vishawishi vya ngono hatimaye waweze kujikomboa kifikra, kiutamaduni na kiuchumi.
Wito huo umetolewa tarehe 05.10.2023, na Diwani wa Kata ya Mbuyuni Mheshimiwa Samwel Msuya, alipokuwa akizungumza na wanafunzi wa kike wa Shule hiyo katika hafla fupi ya Jukwaa la Wanawake wa Kata hiyo ya kuzindua Taulo za Mtoto wa Kike zijulikanazo kama Sanitary Pads.
Mheshimiwa Msuya pia amewataka wasichana kujua thamani yao na kuepuka kutumiwa vibaya na watu wanaotaka kuivuruga safari yao ya maisha.
“Kataa kabisa mawazo ya kukatisha tamaa kwani hofu kama ilivyo furaha huambukiza. Jaribu kuwaepuka marafiki wenye mawazo ya kukatisha tamaa kwani hao ndiyo maadui wakubwa wa maisha yako na wa kukukwamisha kufikia malengo yako,” alisisitiza mheshimiwa Msuya.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa