Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima amewataka waganga wakuu wa Mikoa (RMO) na wa Wilaya (DMO) zote hapa nchini kuanzisha huduma za kipaumbele katika vituo vya Afya ambavyo havijakamilisha ujenzi wa jengo la mama na mtoto zikiwemo huduma za chanjo, kupima akinamama wajawazito na matatizo madogo ya dharura wakati Serikali inajipanga kukamilisha majengo hayo.
Dkt. Gwajima ametoa agizo hilo leo April, 27 wakati wa uzinduziwa wiki ya chanjo Kitaifa iliyofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Chamwino “B” katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.
‘’Tutaanza kulia na jina la Gwajima kwasababu uwezekano wa kufanya vitu upo halafu hatufanyi, matatizo yetu ni mengi na rasilimali ni chache lakini tukijiongeza tutaweza kupunguza tatizo mojawapo hasa matatizo yanayogusa huduma za mama na mtoto’’ amesema Dkt. Gwajima.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare amesema lengo la siku ya chanjo duniani, ni kuelimisha na kuhamasisha jamii juu ya umuhimu wa Afya katika kujikinga na magonjwa yanayozuilika kwa chanjo na kuepuka vifo vinavyoweza kuzuilika kwa njia ya chanjo.
Aidha, Loata Sanare amewaagiza Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi Mkoani humo kuhakikisha wanasimamia zoezi la kuhamasisha wazazi kuwapeleka watoto katika vituo vya afya kwa ajili ya kupata chanjo na Elimu juu ya umuhimu wa chanjo.
Sambamba na hayo, Loata Sanare amebainisha kuwa kuongezeka kwa vituo vya kutolea huduma za Afya Mkoani humo, kumewanufaisha wananchi na kuhakikisha huduma zinawafikia popote walipo ikiwa ni sera ya Rais wa awamu ya sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. SamiaSuluhu Hassan.
Kwa upande wake Mwakilishi kutokaShirika la Afya Duniani – WHO Dkt. William Mwengee ameipongeza Tanzania kwa kutokomeza baadhi ya magonjwa kutokana na ufanisi wa chanjo ambayo imekuwa ikifanyika ikiwemo chanjo ya ugonjwa wa Fulio na Surua.
Dkt. Mwengee amesema WHO itaendelea kutoa ushirikiano na Tanzania katika kutoa huduma za Afya ili kufikia malengo endelevu ya kutoa huduma kwa wananchi ikiwepo huduma ya chanjo mbalimbali.
Mwakilishi kutoka Ofisiya Rais TAMISEMI Bi. Joseline Ishengoma, ametoa wito kwa wazazi kuwapeleka watoto katika vituo vya Afya kwa lengo la kupata chanjo na huduma nyingine kwa kuwa kwa sasa katika vituo vya kutolea huduma za Afya kuna vifaa na watumishi wakutosha wa kutoa huduma hiyo.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa