HALMASHAURI ya Wilaya ya Kibaha Vijijini, imetoa pongezi kwa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kwa utekelezaji mzuri wa miradi ya maendeleo kwa ajili ya Wananchi wa Manispaa hiyo.
Pongezi hizo zimetolewa Machi 03/2023 wakati wa ziara ya Viongozi hao wakiongozwa na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo , Nuru Ndalahwa katika ziara ya kujifunza miradi mikubwa ya maendelea ikiwemo Soko kuu la Chifu Kingalu.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo , Mhandisi wa Mkoa wa Pwani, Charles Kabeho, amesema kuwa kitendo cha Manispaa ya Morogoro kutekeleza miradi ya maendeleo ni moja ya hatua kubwa ya kuhakikisha ya kwamba wananchi wanapata huduma bora.
“Tunawapongeza sana Manispaa ya Morogoro kwa kutekeleza miradi hii mikubwa ya maendeleo, hususani katika mradi huu wa Soko kuu, ni hatua kubwa mno mmeifanya, tumeona mmefanikiwa jinsi ya kuwapanga wafanyabiashara wadogo wadogo, sisi tumekuja kujifunza kutoka kwenu na tunakwenda kutekeleza katika Halmashauri yetu.” Amesema Kabeho.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Vijijini,Nuru Ndalahwa, ameongeza kuwa Manispaa ya Morogoro ina vitega uchumi vingi na kutokana na kujifunza vitega uchumi hivyo wanaweza kufanya vizuri Zaidi yao.
“Naamini kwa kutupokea huku na kukubali tupitie vitega uchumi vyenu ili tuone wenzetu mmefanya vitu gani kwani kimapato mpo juu, tunawapongeza sana na tumeona mmestahili kuwa Manispaa na naamini kwa kijifunza huku tunaweza kufanya vizuri zaidi yenu.” Amesema Ndalahwa.
Naye Kaimu Mkurugenzi Manispaa ya Morogoro Pilly Kitwana, amesema kwa mwaka Manispaa ya Morogoro inakusanya zadi ya Bilioni 11 hivyo kuongezeka kwa vitega uchumi vitasaidia kuongeza Zaidi pato la Manispaa.
Katika ziara hiyo, Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Vijijini, imeambatana na viongozi wafuatao wakiwemo Mhandisi wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi wa Halmashauri ya Wilaya Kibaha Vijijini, Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Mchumi wa Halmashauri, Afisa Masoko , Afisa Biashara pamoja na Afisa Maendeleo ya Jamii.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa