HALMASHAURI ya Jiji la Arusha imetoa pongezi kwa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kwa utekelezaji mzuri wa miradi ya maendeleo kwa ajili ya Wananchi wa Manispaa hiyo.
Pongezi hizo zimetolewa Januari 18/2023 wakati wa ziara ya Jiji hilo la kufanya ziara ya kujifunza namna ya uendeshaji wa miradi mikubwa ya maendelea ikiwemo Soko kuu la Chifu Kingalu na stendi ya Mabasi ya Msamvu.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Meya wa Jiji la Arusha, Mhe. Maxmillian Iraghe, amesema kuwa kitendo cha Manispaa ya Morogoro kutekeleza miradi ya maendeleo ni moja ya hatua kubwa ya kuhakikisha ya kwamba wananchi wanapata huduma bora
“Tunawapongeza sana Manispaa ya Morogoro kwa kutekeleza miradi hii mikubwa ya maendeleo, soko kuu pamoja na kituo cha mabasi cha kisasa Msamvu ni hatua kubwa mno mmeifanya, tumeona mmefanikiwa jinsi ya kuwapanga wafanyabiashara wadogo wadogo, sisi tumekuja kujifunza kutoka kwenu na tunakwenda kutekeleza katika Halmashauri yetu.” Amesema Mhe. Iraghe.
"Hongereni Manispaa ya Morogoro kwa kuwa na miradi ya Kimkakati, tumejifunza mengi lakini kubwa, ni utaratibu wa uendeshaji wa Soko , utaratibu huu ni rahisi sana kupelekea kutokuwepo kwa migogoro baina ya wafanyabiashara na Viongozi" Ameongeza Mhe. Iraghe.
Kwa upande wa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro , Mhe. Paschal Kihanga, amepongeza Jiji la Arusha kwa hatua waliochukua ya kufanya ziara kwani Manispaa ya Morogoro imekuwa chuo cha mafunzo hususani katika miradi ya kimkakati.
Aidha kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Jeremiah Lubeleje, amesema kuwa uamuzi walioufanya wa kujenga kituo cha kisasa cha mabasi Msamvu ni chanzo kikubwa cha mapato kwenye Halmashauri.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa