RAIS Dk John Magufuli amemwagiza waziri wa nchi ofisi ya Rais Tamisemi, Suleiman Jaffo kuhakikisha stendi mpya za mabasi katika halmashauri nchini zinatenga maeneo ya mama lishe,baba lishe na wafanyabishara wadogo wa machinga.
Rais alitoa agizo kwa Waziri huyo kuwa halmashauri za wilaya ambazo haitaonesha kufuata agizo hilo zisipewe fedha za Serikali katika mpango wa ujenzi wa stendi za kisasa nchini.
Agizo hilo alilitoa Mei 6, mwaka huu wakati wa uzinduzi wa mradi wa kituo cha mabasi msamvu, unaosimamiwa na kampuni ya Msamvu Properties Company (T) Limited ambapo mfuko wa LAPF ulisaini makubaliono na Manispaa ya Morogoro.
Alisema kuwa kutokana na mpango mzuri wa mradi wa stendi ya mabasi ya msamvu kuwa wa kisasa na kwa vile serikali imekuwa inatoa fedha za ujenzi wa stendi kama hiyo kwenye halmashauri za wilaya nchini, serikali imeamua kulichukua deni lote lililokuwa ina daiwa na mfuko wa LAPF na kulipwa na serikali.
Alisema kuwa baada ya kukabidhiwa stendi hiyo na LAPF ,Manispaa iweke utaratibu wa kuona kwamba kila mfanyabiashara mdogo anapata nafasi ya kufanya biashara katika kwa kufuata utaratibu na si kuwabagua.
Alisema kuwa amekubali kuja kufungua standi hiyo, lakini hakufurahishwa na kitendo cha kuwabagua ,hivyo ni budi watu wanyonge wathaminiwe kama walivyo wafanyabiasha wakubwa na wakati.
Hata hivyo Rais alishangazwa na taarifa ya LAPF ya makusayo ya kiasi cha sh milioni tatu kwa siku wakati idadi ya ya magari yanayoingia kwa siku ni kati ya 500 -540 na yanalipa ushuru wa sh 2,000 kwa basi moja ukiacha magari madogo.
Rais alisema anadhani kwa idadi ya magari kiwango hicho kinaweza kuongezeka zaidi na jambo hilo analiachia uongozi wa bodi ya uendeshaji wa kituo hicho cha mabasi Msamvu.
Alisema kuwa stendi hiyo ni uwekezaji hivyo utaratibu wa kusimamia makusanyo ya mapato na yataongezeka kutokana na utaratibu utakao wekwa kuruhusu kada zote za wafanyabiashara.
Hata hivyo alisema kuwa, mkoa wa Morogoro umekuwa na bahati kubwa kwa vile upo kati ya Dar es salaam jiji la kibiashara na jijim la Dodoma makao mkuu ya serikali na Ujenzi wa reli ya kisasa yenye mwendo kasi utaifanya uwe wa kimkakati zaidi kukua kwa uchumi wake na wanachi kupata kipato kikubwa.
"wananchi waitumke fursa hii ya jiongrafia iliyopo katika masuala ya kibiashara"alisema Rais.
Hata hivyo ameipongeza halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kwa kubuni mradi huo mkubwa na wakisasa wakuigwa
Naye Mwenyekiti wa bodi, Eliudi Sanga katika taarifa yake ya mradi huo alisema kituo hicho baada ya kukamilika awamu ya kwanza kwa gharama ya sh bilioni 12, kilianza rasmi kazi Novemba 2016.
Alisema awamu ya pili imefanyiwa tathimini ikihusisha ujenzi wa eneo la mabasi ya ndani ya mkoa na eneo lipo hatua za mwisho kukamilika litakuwa na uwezo wa kuegesha mabasi 40.
Mwenyekiti wa bodi hiyo ambaye ni Mkugugenzi mkuu wa mfuko wa LAPFo alisema pia ujenzi wa maduka madogo 80 ulioanza juni 2018 kwa gharama ya sh milioni 768.4 , ambapo pia kituo hicho kimelipa kodi ya serikali sh milioni 152 kuanzia mwaka 2010.
Alisema makubaliono kati ya L APF na Manispaa ya Morogoro umiliki wa hisa ulikuwa ni asilimia 60 kwa Mfuko wakati Manispaa ni hisa ya asilimia 40.
Hata hivyo alisema , wazo la ujenzi wa kituo bora cha mabasi Manispaa ya Morogoro lilianza mwaka 2008 baada ya kuona kuwa kituo kilichokuwepo awali kilikuwa na mapungufu mengi na hakikuwa kinakusanya mapato ya kuridhisha.
Alisema ,mapato ya wakati huo yalikuwa ni wastani wa Sh 350,000 kwa siku na baada ya kuanza kusimamia hivi sasa yamefikia sh milioni tatu kwa siku na kampuni inatarajia kukusanya kiasi cha Sh bilioni 3.11 katika mwaka huu wa fedha 2017/2018 ukilinganishwa na zilizokuwa zikikusanywa Sh milioni 515.5 mwaka 2013.
“ Tunatarajia kuanzia mwaka ujao wa fedha wanahisa wataanza kupata gawiwo” alisema Sanga.
Naye Waziri Jaffo alisema kuwa uzinduzi wa stendi ni mwendelezo ambapo baadhi zimefunguliwa ni stendi tatu ambazo ni Korogwe, Singida na ya Morogoro.
Hata hivyo alisema kuwa ,tayari serikali na wahisani imejipanga kwa kwa ajili ya kujenga stendi za mabasi za kisasa katika halmashsuri nane nchini ikiwemo ya mji wa Songea.
Alisema fedha hiyo ya ujenzi wa stendi ni baada ya Tamisemi kusaini mkataba wenye thamani ya sh bilioni 156 kwa miradi mbalimbali ikiwa ni pamoja na ujenzi wa stendi nane.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa