MKURUGENZI wa Manispaa ya Morogoro, Ally Machela, amesema Manispaa ya Morogoro ipo mbioni kutumia jumla ya Viwanja 3250 kwa ajili ya kutatua migogoro ya ardhi miliki pandikizi kwa ajili ya wananchi ambao walikuwa na migogoro ya ardhi mara baada ya kupatiwa mkopo wa shilingi Bilioni 1kwa ajili ya kutekeleza mradi wa kupanga, kupima na kumilikisha viwanja katika eneo lililokuwa na mgogoro katika shamba la Tungi ( Tungi Sisal Estate).
Hayo ameyazungumza Novemba 18/2021 katika Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kilakala Soko Kuu la Chifu Kingalu Morogoro.
Akizungumza na Waandishi wa habari, Machela, amesema Manispaa ya Morogoro inatarajia kupata Viwanja 6250 kutoka katika ekari 4000 zilizorudishwa kwa wananchi kupitia wawekezaji wa Star City eneo la Tungi Estate.
Machela, amesema kati ya hekari hizo 4000, katika utekelezaji wake , Manispaa ya Morogoro itapata asilimia 45% ya viwanja vitakavyozalishwa na asilimia 55% itabaki kwa Wananchi wa eneo la Star City.
Hata hivyo, amesema kuwa, kupitia viwanja hivyo, jumla ya shilingi 7,466,715,00.00 zinatarajiwa kukusanywa kutokana na mauzo ya viwanja, na hivyo kuipatia faida Manispaa ya Shilingi milioni 6,308,715.00 baada ya kuondoa gharama za uzalishaji.
Amesema faida nyinginezo zitakazo patikana ni ongezeko la makazi yaliyopangika kutoka asilimia 65% ya sasa mpaka 70% ongezeko la wigo wa mapato yatokanayo na kodi ya ardhi na uwepo wa maeneo ya huduma za jamii.
Aidha, amesema kuwa katika Mwaka wa fedha 2021/2022 Manispaa ilitenga bajeti ya shilingi 127,000,000.00 kwa ajili ya kutekeleza shughuli za kupanga na kupima hivyo kupelekea upungufu wa shilingi Bilioni 1,031,000,000.00.
Mwisho, amesema fedha zitakazopatikana kama faida zitaiwezesha Halmashauri kuendeleza shughuli za upangaji , upimaji na umilikishaji wa viwanja katika maeneo mengine ya mji.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa