Jumuiya ya Kiislamu ya Ahmadiyya Morogoro imetoa msaada wa vyakula kwa zaidi ya Kaya 100 zenye uhitaji zilizopo Kata ya Kihonda Maghorofani Manispaa ya Morogoro kuelekea katika Sikukuu ya Eid Fitr.
Akizungumza mara baada ya kukamilika kwa zoezi hilo la ugawaji wa vyakula,DC Msulwa, ameomba mashirika na Taasisi zingine yakiwemo madhehebu ya dini kuelekeza misaada mbalimbali kwa wananchi wenye uhitaji maalumu ili kutengeneza furaha na kudumisha umoja baina yao na wenye uhitaji .
DC Msulwa, ambaye ndiye mgeni rasmi wa hafla hiyo fupi amesema Ahmadiyya wamefanya jambo la uchamungu ambalo linatakiwa liigwe na Taasisi nyingine.
Naye Mkuu wa Chuo cha Jumuiya ya Ahmadiyya Morogoro, Sheikh Abid Mahmood Bhatti, amesema kuwa msaada huo umetolewa kuunga mkono wito wa Serikali inayohimiza mashirika,taasisi,na watu binafsi kutoa misaada kwa jamii yenye uhitaji.
Bhatti, amesema licha ya kuunga mkono Serikali lakini pia kuweza kutoa zakatul Fitri kwa jamii ili kuweza kujumuika na jamii kwa pamoja katika kusherehekea sikuuu ya Eid Fitr inayotarajiwa kuwa katika hizi siku mbili za usoni ambapo itatokana na muandamo wa mwezi.
"Jumuiya ya Ahmadiya ni moja ya sehemu inayojihusisha na utoaji wa misaada mbalimbali ikiwemo ya kiafya,kielimu na kijamii kwa kuwafikia watu wenye uhitaji, hivyo kutoa kwetu chakula kwa watu wenye uhitaji kwanza tumetekeleza misingi ya dini , kwani sisi tumekuwa tukifanya hivi kila ifikapo siku ya Eid basi tumekuwa tukijumuika na ndugu zetu kuhakikisha kwamba tunakuwa nao pamoja katika kusheherekea sikukuu hii " Amesema Bhatti.
Kwa upande wa Diwani wa Kata ya Kihonda Maghorofani, Mhe. Hamisi Ndwata, ameupongeza Uongozi wa Jumuiya ya Kiislamu ya Ahmadiyya Morogoro kwa kuwajali wananchi na kuweza kula pamoja Sikukuu hiyo.
Mhe. Ndwata, amesema Jumuiya hiyo mbali na kugawa vyakula kwa wenye mahitaji , lakini imekuwa mstari wa mbele katika kuchangia mambo mbalimbali ya maendeleo kama vile ujenzi wa madarasa wamekuwa wakijitoa sana.
"Mimi binafsi naridhika sana na ushirikiano wa Jumuiya hii, wamekuwa karibu sana na Jamii lakini hata katika kushiriki mambo ya maendeleo wamekuwa mstari wa mbele sana kuchangia, hivyo nawaomba mwakani panapo uzima wagawe vyakula kwa idadi kubwa ya watu zaidi ya hapa" Amesema Ndwata.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa