KAMATI ndogo ya afya Manispaa ya Morogoro ikiongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhe. Aisha Kitime, imefanya ziara ya kukagua miradi ya afya katika Manispaa hiyo na kutoa pongezi za uendeshaji wa miradi kwa kuzingatia viwango ikiwemo ubora wa majengo pamoja na kasi ya uendeshaji.
Kauli hiyo ameitoa Aprili 11/2023 wakati wa ziara ya kukagua miradi ya afya ikiwamo Zahanati ya Misongeni Kata ya Bigwa , Zahanati ya Kilakala ,pamoja na Zahanati ya Mji Mkuu ambayo inaendelea na ujenzi.
Mhe. Kitime,amesisitiza muda uliopangwa wa uendeshaji wa miradi kukamilika uendelee kuzingatiwa na katika maeneo ambayo yameonekana kuna changamoto yafanyiwe kazi pamoja na kuboresha huduma za afya katika vituo hivyo.
"Tumetembelea miradi yetu ya afya, lengo la kamati hii ndogo ni kusaidia kamati kuu ya afya kufanya kazi kwa urahisi, ,tumeona ubora wa majengo ni mazuri na wauguzi wetu wanajitahidi kuwahudumia wagonjwa, kikubwa niombe kuwasisitiza waganga wafawidhi katika Vituo kuwashirikisha viongozi wenu wa ngazi ya kata kwenye Kila hatua kuepusha kutokea kwa changamoto mwishoni" Amesema Mhe. Kitime.
Mhe. Kitime, amewataka Waganga wafawidhi kuhakikisha katika vituo vyao kuna vifaa tiba vidogovidogo huku wakiendelea kusubiria vifaa vyengine vya huduma.
Hata hivyo, Mhe. Kitime, amemuagiza Mganga Mkuu wa Manispaa kuhakikisha katika Vituo vya afya na Zahanati zinapohitaji wauguzi basi wawapeleke kwa haraka ili huduma ziendelee kutolewa.
Mwisho wajumbe waliendelea kusisitiza katika changamoto zilizopatikana kwenye baadhi ya miradi kutiliwa mkazo kuhakikisha zinafanyiwa kazi ikiwa ni moja ya kazi ya kutimiza majukumu ya kamati.
Manispaa ya Morogoro kupitia mapato yake ya ndani imeshatekeleza ujenzi wa Zahanati 6 kwa mwaka wa fedha 2021/2022 ikiwamo Mbuyuni, Kihonda Maghorofani, Sultan Area, Tungi, Mgaza Mindu, na Kiwanja cha ndege huku Zahanati nyengine zikiendelea na ujenzi.
Aidha, katika mwaka wa fedha 2022/2023 Manispaa inaendelea na Ujenzi wa Zahanati mpya 4 ambazo ni Zahanati ya Kauzeni ambayo kiasi cha shilingi milioni 100 Mazimbu shilingi milioni 135 zimeshaingizwa, Uwanja wa Taifa milioni 50 na Kiyegea B milioni 50 pamoja na Zahanati ya Konga milioni 50 zimeingizwa
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa