MWENYEKITI wa Kamati ndogo ya Mazingira Manispaa ya Morogoro, Mhe. Hamisi Kilongo, akiongozana na Wajumbe wa Kamati hiyo, wamefanya ziara ya kamati hiyo ambapo katika ziara wametembela Kitalu cha Miche kinacho milikiwa na Manispaa ya Morogoro ambacho kinatarajiwa kutembelewa na Mwenge wa Uhuru 2023 Mei.
Akizungumza katika eneo la Kitalu hicho, Mhe. Kilongo, amewataka waangalizi wa eneo hilo kwa kushirikiana na wataalam wa Mazingira kuhakikisha kuwa eneo hilo linapangika vizuri na kuwa safi.
"Huu ni mwenge wa uhuru unakuja hapa, tuhakikishe usafi wa eneo hili unaimarika, na kama kuna changamoto zozote tunamuomba Mkurugenzi kuweka nguvu ya fedha kuhakikisha mradi huo unakidhi vigezo vya kutembelewa na mwenge hatutaki aibu Maafisa Mazingira kuanzia leo hapa kuwe ndio kituo chenu cha kazi ,, tuna muda mchache wa kujiandaa " Amesema Mhe. Kilongo.
Aidha, Mhe. Kilongo,amesema kumekuwa na desturi ya upandaji wa miche shuleni ambapo mingi imekuwa ikipandwa ni miche ya mbao hivyo amesema ipo haja sasa ya kujikita katika upandaji wa miche ya matunda.
Kwa upande wa Mjumbe wa Kamati hiyo ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mwembesongo, Mhe. Ally Kalungwana, amesema licha ya kuwepo kwa miche ya mbao lakini kuna haja ya kuwa na vitalu vya maua ili vitumike katika kupendezesha Mji na kuwauzia wengine wenye uhitaji wa mapambo ya nyumbani.
Kwa upande wa Mkuu wa Kitengo cha udhibiti wa taka na usafishaji, Samwel Subi, amesema katika bustani hiyo watahakikisha kuna vibao vya majina ya miche yote inayo oteshwa pamoja na kuweka njia za kupitika katika bustani hiyo.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa