MWENYEKITI wa Kamati ndogo ya Mazingira Manispaa ya Morogoro, Mhe. Hamisi Kilongo, akiongozana na Wajumbe wa Kamati hiyo, wamefanya ziara ya kamati hiyo ambapo katika ziara walitembelea Kata ya Kihonda Maghorofani pamoja na Kata ya Kihonda.
Ziara hiyo imefanyika Januari 18/2023, ambapo lengo la ziara hiyo ni kuangalia changamoto za usafi katika Kata ya Kihonda Maghorofani baada ya kupata malalamiko juu ya mzabuni wa usafi Kata hiyo na kutembelea Kata ya Kihonda kuangalia eneo lililopita mkondo wa maji unaosababisha mafuriko wakati wa mvua Kata ya Kihonda.
Katika Kuona namna gani ya kutatua kero ya usafi Kata ya Kihonda, Kamati ilimtaka mzabuni wa usafi wa Kata ya Kihonda Maghorofani ambaye ni Kajenjere kuonesha taarifa za madeni wanazowadai wananchi lakini kufanyia kazi malalamiko ya wananchi katika uzoaji wa taka kwa wakati.
"Tumepokea malalamiko kutoka kwa Diwani wa Kata hii kufuatia wananchi kumlalamikia ucheleweshwaji wa uzoaji wa taka, sasa kama kamati kwanza tumemtaka mzabuni Kajenjere kuyafanyia kazi malalamiko ya wananchi, lakini kutuletea taaria ambazo wanadai kuwa wananchi wa Kata hiyo wanadaiwa baada ya hapo sasa tutakaa kuona namna bora ya sisi na wao jinsi ya kufanya kazi, tunataka Mji wetu uwe safi, taka zikizagaa hvyo zitaleta magonjwa ya mlipuko, " Amesema Mhe. Kilongo.
Kwa upande wa Mjumbe wa Kamati hiyo,ambaye ni Diwani wa Kata ya Mbuyuni, Mhe. Samwel Msuya, amewataka wazabuni wa usafi pamoja na vikundi kazi vilivyopewa dhamana ya usafi wafanye kazi kwa kuzingatia mikataba waliyosaini ili kuhakikisha Mji wetu unakuwa safi.
Katika hatua nyingine, Mhe. Kilongo ambaye ni Diwani wa Kata ya Kihonda, alifika Kata ya Kihonda Januari 18/2023 akiongozana na Wajumbe wa Kamati ndogo ya Mazingira kuwaona wahanga na kutoa Msaada wa Unga wa Sembe ikiwa ni jitihada za kuwasaidia wananchi hao walio atharika sana na mafuriko na kupotelewa na vitu na kukosa mahitaji muhimu ya kibinadamu.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa