WAJUMBE wa Kamati ya fedha na Uongozi Manispaa ya Morogoro, wameridhishwa na utekelazaji wa miradi ya maendeleo, inayotekelezwa na fedha za Umma .
Hayo yamesemwa Mei 18/2022 katika ziara ya kamati hiyo baada ya kutembelea miradi ya maendeleo ikiwepo Kituo cha Afya Kata ya Lukobe, Jengo ambalo linahitaji kuendelezwa kuwa Zahanati Kata ya MjiMkuu, Shule mpya ya Sekondari Kata ya Mindu ambayo ujenzi wake umefikia asilimia 72 pamoja na kukagua fremu zilizopo Soko Kuu la Chifu Kingalu kwaajili ya kuangalia mwenendo wa ulipaji wa kodi kwa wafanyabiashara.
Aidha Wajumbe hao wamefurahishwa zaidi na utekelezaji wa miradi ya maendeleo, huku wakiwataka wataalamu kuongeza nguvu ili miradi hiyo ikamilike kwa wakati.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, mwakilishi wa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Salma Mbandu, amebainisha kuwa, Kamati hiyo ya Fedha, imeridhishwa na hali ya miradi yote iliyotembelewa na kuongeza kuwa hii ni kuonesha kazi nzuri inayofanywa na Serikali ya awamu ya sita, inayoongozwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan.
"Miradi ni mizuri, imetekelezwa kwa viwango na ubora unaokubalika, imetekelezwa kwa kuzingatia Ilani ya Chama cha Mapinduzi pamoja na maelekezo yanayotolewa na Serikali, ikiwa na lengo la kuwahudumia wananchi wote bila kujali itikadi zao, tunapongeza sana juhudi za Mhe. Rais, Mama yetu Samia Suluhu Hassan" Amesema Mhe. Mbandu.
Naye Mjumbe wa kamati hiyo ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mwembesongo, Mhe. Ally Kalungwana, amesema kuwa, utekelezaji wa miradi hiyo, unapambanua juhudi za serikali ya awamu ya sita kisekta, kwa kupanua wigo katika sekta ya elimu kwa kujenga vyumba vya madarasa pamoja na kuongeza vituo vya afya hususani Manispaa ya Morogoro ambapo kwasasa kuna Vituo vya afya 2 ambavyo vipo katika hatua za ujenzi.
Kuhusu, mwenendo wa kodi za waliopanga katika fremu za Soko Kuu la Chifu Kingalu, Mhe. Zamoyoni Abdallah, amesema wadaiwa sugu wote wapewe barua za notes ilikuongezewa muda wa kulipa madeni na kama watashindwa basi maeneo hayo yatangazwe upya ili Soko liweze kujiendesha kupitia kodi za wafanyabiashara.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa