Kamati ya Fedha na Uongozi ya Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro imefanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika kata ya kichangani,kauzeni na Sultani Area.
Katika ziara hiyo wajumbe pamoja na wataalamu kutoka halmashauri walitembelea maendeleo ya ujenzi wa barabara za Tubuyu(k.m 2.4),Nanenane (km.1.6) na Maelewano(km.0.6),sambamba na ujenzi wa kituo cha wanafunzi wenye mahitaji maalumu kata ya Kauzeni.
Akizingumza wakati wa ziara hiyo Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha ambae pia ni Mstahiki Meya Mhe.Pascal Kihanga ametoa pongezi kwa wataalamu kwa usimamizi mzuri wa miradi mbalimbali inayotekelezwa ndani ya Manispaa ya Morogoro.
Aidha Kamati imemtaka Mhandisi wa Manispaa Ndg.Juma Gwisu kumsimamia mkandarasi anaejenga barabara za Tubuyu,Nanenane na Maelewano ambae ni Group Six ,ili aweze kumaliza kazi kwa wakati kama ilivyopangwa katika mkataba.
Kamati ya Fedha na uongozi pia ilikagua ujenzi wa vyumba vya wanafunzi wenye mahitaji maalumu katika shule ya msingi Kauzeni na kutoa pongezi kwa uongozi wa shule ,Afisa Elimu Msingi na Mhandisi kwa kubuni mradi huo na hatimaye kuletewa fedha za utekelezaji wa mradi huo.
Ilielezwa kuwa lengo la mradi huo ni kuweka mazingira ya mazingira ya kujifunzia na kufundishia kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu na kuondoa adha ya kutumia chumba kimoja kama darasa,jiko na bwalo.Mradi huo hadi kukamilika utagharimu kiasi cha Tsh 146,600,000.00 fedha zilizotolewa na katika Wizara ya Elimu,sayansi na Teknologia kupitia mradi wa lipa kulingana na matokeo(Education perfomance for Result -EP4R).Alieleza Ndg. Juma Gwisu.
Hii ni mojawapo ya ziara za ukaguzi wa miradi zinazofanywa na kamati mbalimbali kwa lengo la kuboresha na kufatilia utekelezaji wa miradi mbalimbali.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa