KAMATI ya Huduma za Uchumi, Elimu na Afya Manispaa ya Morogoro ikiongozwa na Mwenyekiti wake , ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Kingo, Mhe. Amini Tunda, pamoja na timu ya wataalamu ya Wakuu wa Idara na Vitengo imetembelea baadhi ya miradi ya Maendeleo ambayo inatarajiwa kupitiwa na Mwenge wa Uhuru Mei 2023.
Akizungumza katika ziara hiyo, Mwenyekiti wa Kamati , Mhe. Amini Tunda, amewataka wataalamu kuhakikisha miradi yote ambayo itapitiwa na Mwenge iwe katika viwango na kukamilika kwa wakati.
"Siku zimekwisha, tukimbizane na miradi yetu, miradi ni mizuri sana na ya uhakika,kikubwa hizi siku za usoni twendeni kwa spidi ,lakini niendelee kuwapongeza wataalamu wetu mmeitendea haki miradi yetu, naamini miradi hii ikimalizika itazidi kutoa huduma kwa wananchi lakini kuwa vyanzo vya mapato yetu ya ndani" Amesema Mhe. Tunda.
Kwa upande wa Wajumbe wa Kamti hiyo kwa pamoja wameridhika na miradi hiyo na kutoa pongezi kubwa Baraza la Madiwani kwa kupitisha matumizi ya fedha za miradi hiyo huku wakitoa pongezi kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro kwa kushirikiana na Wataalamu wake.
Miongoni mwa miradi ambayo Kamati imeitembelea ni Ujenzi wa Shule ya Ghorofa ya Sekondari iliyopo Kata ya Boma yenye gharama ya ujenzi wa Bilioni 1.2, Kituo cha Afya Tungi chenye thamani ya Bilioni 1.2 pamoja na Jengo la Utawala Shule ya Sekondari Mkundi ambapo mpaka sasa jumla ya shilingi milioni 50 zimeshatumika na ujenzi unaendelea.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa