Kamati ya kudumu ya bunge ya hesabu za serikali za mitaa LAAC imeitaka Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kuandaa taarifa ya hesabu za miradi ya maji na barabara nakwamba muda wowote itaitwa mbele ya kamati hiyo bungeni ajili ya kuhojiwa.
Agizo hilo lilitolewa na mwenyekiti wa kamati hiyo ya kudumu ya bunge Vedasto Ngombale Mwilu baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa kituo cha kutega na kuchujamaji pamoja na tanki la kutibu maji ya mseleleko kutoka mto Vituli yanayotumiwana wananchi wa kata ya bigwa na kingolwira manispaa ya Morogoro.
Mwenyekiti huyo wa kamati alisema kuwa mazingira ya kwenye chanzo hicho cha maji hayaridhishi na hayako kwenye usalama kwa kuwa hakuna uzio wala ulinzi wa uhakika hivyo aliwataka MORUWASA ambao kwa sasa wanasimamia mradi huo kujenga uzito nakuimarisha ulinzi.
Alisema kuwa kamati hiyo imekuwa ikifanya kazi baada ya kupokea taarifa kutoka kwamdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali CAG.
Hivyo pamoja na mambo mengine kuhusu mradi huo CAG katika taarifa yake aliyowasilisha kwa kamati hiyo alieleza changamoto za mradi huo ikiwemo ya wananchi kupasua mabomba kwa makusudi kwa lengo la kupata maji.
“Kitendo hicho cha wananchi kupasua mabomba kwa makusudi kinazua tafsiri huwenda wananchi waliokuwa jirani na chanzo wanakosa maji na ndio maana wanaamua kupasua mambomba hayo kama njia ya kukomoa wenzao wanaonufaika na maji yachanzo hicho” alisema Ngombale Mwilu.
Akijibu changamoto hiyo Mkurugenzi wa MORUWASA Mhandisi Nicholaus Angumbwike alisema tangu mamlaka hiyo imepokea mradi huo haijawahi kupata taarifa ya kupasuliwa kwa mabomba kwa makusudi isipokuwa inatokeaga mivujo ya kawaida hata hivyo aliahidi kuzifanyia kazi taarifa hizo.
Naye kaimu mhandisi wa maji wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro Edward Kisalu alisema kuwa mradi ulitarajiwa kuwanufaisha wananchi 8264 lakini kwa sasa kumekuwa na ongezeko kubwa la watu.
Alisema kuwa mradi huo ulianza mwezi desemba 2014 na ulikamilika Juni 2015 na uligharimu zaidi ya Sh mil 500 fedha ambazo zilitoka serikali kuu kupitia mfuko wa pamoja wa maendeleo ya sekta ya maji.
Mmoja wawabunge wa kamati hiyo Costantine Kinyaso alieleza wasiwasi wake kuhusu usalamana usafi wa maji kwenye chanzo hicho ambacho kiko jirani na wananchi wanaofanyashughuli mbalimbali za kibinadamu.
“Huku juu mlimani kwenye chanzo kuna makazi ya watu na wamejenga vyoo ambavyo viko jiranina mto, Halmashauri hebu angalieni namna ya kuwasogeza hawa wananchi waliokuwa ndani ya hifadhi ya mto vinginevyo maji haya yanaweza yasiwe salama,” alisema Kinyaso.
Kamati hiyo pia ilikagua mradi wa barabara ya Mei mosi yenye urefu wa kilometa 5.1 ambayo ujenzi wake umegharimu Sh 11.8 bilioni na barabara yaTubuyu-nanenane- maelewano yenye urefu wa kilometa 4.6 ambayo ujenzi wake umegharimu Sh. 12.6 bilioni fedha ambazo ni mkopo kutoka benki ya dunia.
Kwa upande wake Meya wa Manispaa ya Morogoro Pascal Kihanga alisema kuwa ujio wa kamati hiyo katika manispaa umempa faraja kwani kwa muda mrefu kumekuwa namaneno na shutuma nyingi dhidi yake zilizokuwa zikitokewa na baadhi ya watu wakiwemo viongozi kuhusu mradi wa ujenzi wa barabara ya Tubuyu-Nanenane-Maelewano.
“Maneno mengi yamezungumzwa lakini nashukuru kamati hii imekuja kushuhudia kwa kuona nakujiridhisha na sasa wanaweza kupima na kubaini ukweli wa maneno yaliyokuwa yakizungumzwa,” alisema Kihanga.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Regina Chonjo aliahidi kutumia sheria za mazingira ili kutoa elimu kwa wananchi wanaoishi jirani na vyanzo vya maji.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa