KAMATI ya Mipango Miji na Mazingira Manispaa ya Morogoro, inayoongozwa na Mhe. Ally Kalungwana, ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mwembesongo,imefanya ziara kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ndani ya Manispaa ya Morogoro .
Ziara hiyo imefanyika Aprili 12/2023 ikiambatana na Wakuu wa Idara na Vitengo ambapo Wajumbe hao walipata nafasi ya kila mmoja kuchangia hoja juu ya Kamati hiyo.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhe. Ally Kalungwana, amesema kuwa imefika sasa wakati wa wananchi wasiorasimishiwa warasimishiwe na wale ambao washalipia zoezi la urasimishaji waangaliwe ili wapate haki zao za msingi na kuweza kumiliki ardhi.
"Serikali inaendelea na program ya kupanga na kupima ardhi ikiwa na lengo la kuondoa makazi holela, hivyo niombe zoezi hili liendelee ili kupunguza migogoro ambayo imekuwa ikiwakosesha raha wananchi na kufanya Serikali kila uchwao kusilikiza kesi za ardhi jambo ambalo kwa mji unaoendelea unaotakiwa kuwa Jiji sio jambo lenye afya" Amesema Kulungwana.
Katika ziara hiyo, Wajumbe wa Kamati hiyo walitaka zoezi la urasimishaji ambalo lilionekana kusimama liendelee kwani kila sehemu kumekuwa na malalamiko ya urasimishaji .
Aidha, wajumbe hao, wamewataka wananchi kuhakikisha wanalipia gharama za urasimishaji ili waweze kupatiwa hati kwa lengo la kupunguza migogoro ya ardhi na kutaka uhamasishaji zaidi kutoka kwa viongozi mbalimbali.
Baada ya ziara hiyo kumalizika wajumbe wote waliongozana na kuelekea katika ukumbi kwa ajili ya kufanya majumuisho ya ziara hiyo.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa