KAMATI ya Kudhibiti UKIMWI Manispaa ya Morogoro ikiongozwa na Naibu Meya wa Manispaa , Mhe. Mohamed Lukwele, imesema itajikita zaidi katika kupunguza maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI.
Kauli hiyo,ameitoa Oktoba 17/2022 katika ziara ya kamati hiyo ya kutembelea baadhi ya wadau wanaojihusisha na masuala ya UKIMWI ikiwa ni lengo la kujifunza ni kwa namna gani Manispaa ya Morogoro itaweza kupunguza kwa kiasi kikubwa maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI.
Kamati imeweza kupata taarifa fupi ya kwa namna gani Manispaa imeweza kudhibiti kwa kiasi kikubwa maambukizi mapya ya UKIMWI na wameweza kutembelea Taasisi ya Wezesha Mabadiliko iliyopo Kata ya Uwanja waTaifa kwa lengo la kujua jinsi wadau walivyojipanga katika kupunguza maambukizi mapya ya Virusi vya UKIMWI.
Mhe.Lukwele, amesema kuwa kufanya ziara hizo ni moja ya kujiwekea malengo ya Manispaa kuendelea kuweka mipango thabiti ya kumaliza kabisa maambukizi mapya.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro ambaye pia ni Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Morogoro, Faraja Maduhu, amewaomba wadau wa masuala ya UKIMWI kujitokeza zaidi ili kuweza kupunguza changamoto zinazowakabili kwani wadau waliopo hawatoshi kufikia vituo vyote vya kutolea huduma.
Kwa upande wa Maratibu wa kudhibiti UKIMWI , Manispaa ya Morogoro, Upendo Elias, ameishukuru Kamati kwa ziara hiyo kwani itasaidia sana wadau nawao kuweza kujifunza ili kujua wapi waongeze na wapi kwa kupunguza ili waweze kufikia lengo la kudhibiti maambukizi mapya ya UKIMWI.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa