Kamati ya Ushauri Wilaya imeridhia na kupitisha jumla ya Tsh 75,372,267,796.32 ikiwa ni mapendekezo ya bajeti ya mwaka wa fedha 2020/2021 ikijumuisha mapato ya Ruzuku na mapato ya ndani.
Hayo yamebainishwa na Mchumi wa Manispaa Sadoth Kaijage wakati akiwasilisha bajeti ya Halmashauri katika kikao cha kamati ya ushauri wilaya kilichofanyika leo Februari 7 katika ukumbi wa mikutano.
Ameeleza kuwa katika mwaka wa fedha 2020/2021 Halmashauri inakisia kukusanya kiasi cha Tshs 8,478,799,224.32 ambapo Tsh 498,870,893.41 ni uchangiaji wa huduma za afya na Tshs 271,759,000.00 ni uchangiaji wa ada za wanafunzi kutoka katika vyanzo vya ndani na kiasi hicho ni ongezeko la Tsh 1,772,873,011.45 ambayo ni sawa na asilimia 26.43 ya makadirio ya mwaka 2019/2020 ya Tshs 6,705,926,212.87.
Aidha katika mwaka wa fedha 2020/2021 Halmashauri inatarajia kupokea kiasi cha Tsh 7,483,018,572 kutoka Serikali kuu na wahisani mbalimbali kwaajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ambapo Serikali kuu wanatarajia kuchangia kiasi cha Tsh 5,832,810,000 na Tsh 1,650,208,572 ikiwa ni fedha za nje.
Pia ameeleza kuwa katika mwaka wa fedha 2020/2021 Halmashauri inatarajia kutumia kiasi cha Tsh 59,410,450,000.00 kutoka Serikali kuu kwaajili ya matumizi ya kawaida ya mishahara na matumizi mengineyo ambapo matumizi kwaajili ya matumizi mengineyo yanakisiwa kuwa Tsh 2,495,867,000.00 na itapokea kiasi cha Tsh 2,495,867,000.00 ikiwa ni ruzuku ya matumizi ya kawaida na kati ya hizo Tsh 89,196,000.00 ni fidia ya vyanzo vilivyofutwa.
Akiendelea kuwasilisha mapendekezo ya bajeti Ndg Kaijage ameelezea mikakati iliyowekwa ya kuhakiksha mapato yanakusanywa katika mwaka ujao wa fedha ni pamoja na kupitia upya mifumo ya usimamizi na ufuatiliaji wa mapato kwa kuboresha maeneo ambayo yana mapungufu,kuendelea kuwashirikisha wadau mbalimbali katika kukusanya mapato,kufanya ukaguzi wa mara kwa mara ili kubaini mianya inayovujisha mapato,kupitia upya sheria ndogo za mapato na kutumia mifumo ya ki-electronic katika vyanzo vyote vya mapato.
Akichangia hoja mmoja wa wajumbe wa kikao hicho Ndg Ismail Ismail ameipongeza Halmashauri kwa ujenzi wa soko la kisasa sambamba na ukarabati wa mto kikundi na kushauri eneo la kikundi palipouzwa viwanja kuna eneo lilibaki lijazwe kifusi na litumike kama stendi ya bajaji ili kusaidia usafiri kwa wafanyabiashara na wanunuzi watakaokuwa wanafika kupata bidhaa mbalimbali katika soko hilo.
Naye Ndg. Elizeus Rwegasira alitoa ushauri wa kupunguza bei pendekezwa ya vioski vya soko kuu ambapo vioski vya juu vimependekezwa kulipiwa Tsh 200,000.00 na vya chini Tsh 300,000.00 na kueleza endapo bei itakuwa kubwa wananchi watashindwa kupanga na vitabaki wazi na kuifanya Halmashauri kukosa mapato.
Aidha Mwenyekiti wa CCM Wilaya Ndg Fikiri Juma ameshauri utengenezwe utaratibu wa kuvua samaki katika bwawa la Mindu ili Halmashauri iweze kutoza wavuvi kwa utaratibu mzuri na kuepusha migogoro,na kushauri kijengwe kituo cha polisi katika kata ya Kihonda ambacho kitatoa huduma na hii ni kutokana na wingi wa wananchi wanaoishi katika kata hizo za pembezoni.
Mstahiki meya wa Manispaa amehahidi kuendelea kufuatilia urejeshwaji wa stendi ya Mabasi Msamvu ili Halmashauri iendelee kukusanya na hatimaye kuweza kuendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya kimaendeleo na kwasasa kinachosubiriwa ni ushahidi wa picha za video zilizorekodiwa wakati akitoa tamko hilo.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa