Kanisa la Wadventista Wasabato Jimbo la Kusini mwa Tanzania leo tarehe 3/10/2019 limetoa mapipa 24 ya kuhifadhia takataka yenye thamani ya Tsh mil sita kwa uongozi wa Manispaa ya Morogoro kwaajii ya kusaidia ukusanyaji wa taka ili kuendelea kuuweka mji katika hali ya usafi na mazingira yanayopendeza.
Akikabidhi msaada huo kwa Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Regina Chonjo,Askofu wa kanisa hilo Joseph Mugwabi ameeleza kuwa wao kama kanisa wameona ni vyema kuisadia Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro katika suala zima la usafi wa mazingira na wameamua na hivyo kufikia maamuzi ya kutoa mapipa hayo.
Akipokea msaada huo DC Chonjo amewashukuru kwa msaada huo na kumuagiza Mkurugenzi wa Manispaa kuendelea kutengeneza mapipa mengine yatakayowekwa katika maeneo mbalimbali ya mji ili kuepuka wananchi kuendelea kutupa takataka hovyo.
Aidha Chonjo ametoa wito kwa wananchi kuyatumia mapipa hayo kwaajili ya kutupia takataka na kuacha tabia ya kuyaiba na kuyafanya chuma chakavu na kueleza hatua kali zitachukuliwa kwa mwananchi atakayebainika kufanya uhalifu wowote.
Naye Afisa Mazingira na udhibiti wa taka ngumu Manispaa Samwel Subi ameeleza kuwa mapipa hayo ya kuhifadhia takataka yatawekwa katika maeneo yenye mikusanyiko ya watu kama eneo la Stendi ya Msamvu,stendi za daladala,ofisi kuu ya Manispaa na katika barabara kuu.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa