KATA ya Kilakala Manispaa ya Morogoro imezindua Kampeni ya upandaji wa miti 2000 ikiwa na lengo la kuhakikisha Kata hiyo inakuwa na uoto wa asili.
Kampeni hiyo imezinduliwa na Naibu Meya wa Manispaa ya Morogoro kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya, Mhe. Mohamed Lukwele, leo Februari 19/2022 katika Soko la Kilakala.
Akizungumza wakati wa kampeni hiyo, Mhe. Lukwele, amesema kampeni hiyo inalengo la kuwafanya wananchi waone zoezi la upandaji miti ni sehemu ya maisha ili kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi.
Kuhusu kushirikisha wanafunzi katika kampeni hiyo, Mhe. Lukwele, amesema , Kata ya Kilakala ina shule nyingi hivyo kila mwanafunzi mmoja akipanda mti wake itasaidia katika kukabiliana na changamoto hizo za kimazingira ikiwemo ukame na uhaba wa maji.
“Tumewaita wanafunzi ili muone zoezi la kupanda miti liwe sehemu ya maisha yenu shuleni, kampeni hii tunataka kila mwanafunzi ajivunie mti wake alioupanda na tutaona fahari kubwa kuwa wanafunzi weyu wanajali mazingira na tunajali nchi yetu,ukiona mvua hazinyeshi kwa wingi ujue ni mbadiliko ya tabianchi kutokana na kukosekana kwa miti ” Amesema Mhe. Lukwele.
Mwisho, Mhe. Lukwele, amewashukuru na kuwapongeza wadau mbalimbali ikiwamo SAT waliowezesha upatikanaji wa miti, Morogoro Women Voice and Connection , Ofisi ya Mazingira Manispaa ya Morogoro, Raleigh Tanzania, Wanawake na Mazingira, Moro kwanza Mazingira ,Viongozi wa vyama vya siasa, Wenyeviti wa Mitaa, Watendaji , Waalimu na wanafunzi pamoja na wananchi kwa kushiriki kikamilifu katika kampeni za upandaji miti.
Kwa upande wake, Katibu wa CCM Kata ya Kilakala, Bi. Scholastica Mwanyika , amesema amesemam zoezi kampeni hii ina umuhimu kwa sababu inalenga kuwafundisha wananchi juu ya kupanda miti.
Mwanyika , amesema kama Chama watahakikisha wanaendelea kusimamia vyema suala la mazingira kama Ilani ya CCM ya mwaka 2020-2025 inavyoeleza.
Naye Diwani wa Kata ya Kikalaka, Mhe. Marco Kanga, amempongeza Naibu Meya kwa kuzindua kampeni hiyo na kuahidi kuitekeleza.
Kanga, ameagiza shule zote za Kilakala kuhakikisha wanaitekeleza kwa vitendo pamoja na kuanzisha au kufufua klabu za mazingira ngazi ya msingi na sekondari ambayo amesema ni sehemu ya masomo.
Amesema kuwepo kwa Klabu za mazingira shuleni zitasaidia kuwafundisha vijana kupambana na athari za mabadiliko ya tabanchi na uharibifu wa mazingira kwa ujumla kwa vitendo.
"Leo tumezindua kampeni ya upandaji wa miti, tuna hatua tumezichukua kuendeleza kampeni hii ikiwamo kulinda uoto wa asili, kuendeleza utunzaji wa mazingira, kila mwanafunzi apande mti wake, shule zote kuwa na klabu za mazingira, Kila Taasisi Kilakala kupanda miti , upandaji wa miti kwa kila kaya, kwa kufanya hivyo tunaamini uoto wa asili utarejea katika Kata yetu" Amesema Kanga.
Pia, Diwani wa Viti Maalum , Mhe. Mwanaidi Ngulungu, amesema anaunga mkono kampeni hiyo kwa kuwagusa moja kwa moja wanafunzi kwani inawajega wanafunzi kupenda mazingira.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa