Mkuu wa Wilaya ya Morogoro,Mhe. Regina Chonjo, amewaasa madereva wa pikipiki maarufu kama bodaboda ,kulipia vitambulisho vya wajasiriamali na endapo watashindwa kufanya hivyo hawataruhusiwa kufanya biashara ya kubeba abiria.
Kauli hiyo ameitoa leo Juni 8, 2020 wakati wa kuwakabidhi Vitambulisho vya Wajasiriamali Umoja wa Bodaboda Stendi ya Mabasi Msamvu (BOMSATE).
Akizungumza na madereva hao na kusema ,wao ni moja ya kundi ambalo linapaswa kuwa na vitambulisho vya wafanyabiashara wadogo ambapo wanatakiwa kulipia shilingi 20,000.
Chonjo, amesema kuwa agizo la watu wanaofanyabiashara ambayo mtaji wake hauzidi kiasi cha sh.milioni nne wanapaswa kuwa na vitambulisho hivyo.
“Mnapaswa kununua vitambulisho hivyo na kwa wale ambao hawatakuwa na vitambulisho hivyo hawataruhusiwa kufanya biashara hiyo hivyo hakuna budi kila mmoja wetu kuhakikisha analipia kiasi hicho ili waweze kufanya kazi bila ya usumbufu,” Amesema Chonjo.
Aidha, amewataka wafanyabiashara wengine nao kulipa ili wapatiwe vitambulisho ambavyo Rais ametaka wajasiriamali wadogo wawe navyo kwani nao wanachangia uchumi wa taifa.
“Tunaendelea kuwahamasisha wajasiriamali wadogo wachangamkie fursa hiyo kwani ushuru waliokuwa wakilipa kwa sasa utakuwa haupo na kitambulisho hicho ndicho kitakuwa kimefidia na haitaruhusiwa kufanya bishara kama hawana vitambulisho hivyo,” Ameongeza DC Chonjo.
Kwa upande wa waendesha bodaboda Yustine Mkude, amemshukuru Mhe. Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kuwapatia vitambulisho hivyo huku akisema vimewaondolea usumbufu katika kufanya kazi zao za kutafuta ridhiki.
"Tunamshukuru sana Rais wetu Mhe. Dkt John Pombe Magufuli, kwakweli amefanya jambo zuri la kutukumbuka sisi wanyonge, kwani tumekuwa tukifnaya kazi zetu vizuri bila kusumbuliwa , lakini nimshukuru Mkuu wa Wilaya mama yangu Rgina Chonjo kwa kuitika wito wetu kuja kushiriki kutupatia vitambulisho bila kumtuma mwakilishi hii imeonesha ni jinsi gani Serikali ilivyo karibu na Wananchi wake, tunatoa pongezi tena kwa Mkurugenzi wa Mnaispaa ya Morogoro na Timu yake kwa uhamasishaji mzuri wa Vitambulisho hivi" Amesema Mkude.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa