Kata za Mafiga na Tungi, zimeibuka vinara katika kufanya sherehe za maadhimisho ya siku ya afya na lishe duniani.
Kata hizo zimetajwa Agosti 16-2024 katika kikao Cha kawaida Cha Kamati ya Tathmini ya lishe Manispaa ya Morogoro kilichofanyika Ukumbi wa Manispaa ya Morogoro.
Akizungumza wakati wa ugawaji wa zawadi kwa washindi hao, Mkuu wa Kitengo cha Lishe Manispaa ya Morogoro,Ester Kawishe, amesema Kata hizo zimefanya vizuri sana hususani katika uhamasishaji wa ushiriki wa wanaume kwenye maadhimisho hayo.
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Hilary Sagara, amesema Kata zote ziige Kata hizo mbili katika ushirikishwaji wa wanaume kwenye maadhimisho ya Siku ya Lishe na afya ili elimu ya lishe isambae zaidi kuanzia ngazi ya familia na Jamii kwa ujumla.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa