Mhe.Samia H. Suluhu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, amewataka wananchi kuendeleakulinda amani na umoja kwa ajili ya kujengaTaifa.
Kauli hiyo,ameitoa Julai 7/2021 ,wakati akizungumza na wakazi wa Halmashauri ya Manispaa yaMorogoro katika eneo la Stendi ya Mabasi Msamvu.
Mhe.Samia, amesema wapo watu wanaleta vurugu jambo ambalo halina afya kwa nchi hii nakusababisha kuchelewa kupata maendeleo.
Aidha,amesema changamoto zote zikiwemo za ardhi, biashara ,elimu, maji na miundombinuSerikali ipo makini na tayari hatua zimeshachukuliwa ili wananchi waendelee kupatahuduma bora.
Amesemakuwa Serikali itahakikisha kuwa inatekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCMkwa vitendo ili yale yote yaliodhamiriwa kufanyika yanafanyika na kuleta matunda.
"Serikalitunatekeleza Ilani ya CCM kwa asilimia kubwa, tuna miradi mikubwa tumeshaanza kuitekelezana inaendelea vizuri, tayari huduma za afya, maji , miundombinu tumeshaanzakuboresha kwa asilimia kubwa, niwaombe sana Viongozi mliopewa dhamana fanyeni kazina kutoa huduma bora kwa wananchi ambao wana matumaini makubwa na Serikali yao,imarisheni ulinzi na usalama ili Taifa letu liendelee kuwa nuru kubwa ya amani Afrikanzima na Duniani kote, Taifa likiingia katika machafuko hata hayo maendeleo tunayoyatakasasa hatutayapata tena" AmesemaSamia.
"Leonimepita kuwasalimia, kuwaona na kutambuana, sio ziara yangu rasmi ya kikazi,kama Mkuu wa Mkoa alivyoniomba kuja kufanya ziara , niwaahidi nitarudi kufanyaziara Mkoa huu ili tuzungumze kwa pamoja na tuone jinsi gani tunavyoweza kushirikianakusongesha Taifa mbele kimaendeleo" Ameongeza Mhe. Samia.
Naye Mkuuwa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Martine Shigela, amempongeza Rais Samia, kwa kuipatiaMkoa wa Morogoro miradi mikubwa ya Kimkakati.
Shigela,amesema kwa kushirikiana na Viongozi wa Mkoa wa Morogoro watahakikisha miradi hiyoya kimkakati inafanya kazi na kuendelea kuwahudumia wananchi.
"Tunashukurusana kwa ujio wako Mhe. Rais, wana Morogoro wanaimani kubwa sana na wewe ,tunaomba ufike kufanya Ziara ili wananchi hawa wakusikie na kupokea maagizo yako,Manispaa yetu ya Morogoro tunatamani siku moja iwe Jiji, lakini tunaamini hilo linawezekanakama tukiendelea kujipanga vizuri na kila mtu akafanya kazi kwa nafasi yake" Amesema Shigela.
Katikahatua nyingine, amempongeza sana Rais Samia kwa kukutana na Wananchi wa Manispaaya Morogoro na kumuomba kutenga muda wa kufanya ziara katika Mkoa wa Morogoro ambapoRais Samia amekubali ombi hilo.
Kwa upandewa Kaimu Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Morogoro, Fikiri Juma, amemuomba Mhe. Rais kusaidiakuweza kufufua Viwanda vilivyokufa Manispaa ya Morogoro kwani asilimia kubwa yaViwanda hivyo vilikuwa vinatoa ajira kwa wananchi.
Fikiri,amesema asilimia kubwa ya wananchi wa Mkoa wa Morogoro ajira kubwa wanategemea Viwandakatika kuendesha maisha yao.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa