Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro inatarajia kuanzisha mchakato wa kupitia upya sheria zake ndogo kwa lengo la kuziboresha ili ziweze kuwaletea wananchi maendeleo kulingana na wakati uliopo, imefahamika.
Meya wa Manispaa ya Morogoro, Pascal Kihanga alisema hayo wakati wa kikao cha kawaida cha baraza la Madiwani kilichofanyika tarehe 27/10/2017 katika ukumbi wa halmashauri mjini Morogoro.
Kauli ya Meya huyo ilifuatia hoja iliyowasilishwa na Diwani wa Kata ya Chamwino, Dismas Makanjira , aliyohoji tozo kubwa la sh: 6,000 la uzoaji taka majumbani unaofanywa na halmashauri kupitia vikundi vya uzoaji wa taka ngumu.
“ Naomba sheria ndogo ya uzoaji taka ngumu ifanyiwe mabadiriko na wananchi washirikishwe kuweka viwango vya tozo kwani inayotumika kwa sasa ni kubwa” alisema Makanjira.
Nao baadhi ya Madiwani kwa nyakati tofauti waliutaka uongozi wa Manispaa kuharakisha malipo kwa vikundi vya usafi vya ukusanyaji wa taka ngumu ili kuepuka udanganyifu wa mapato kwa kuwa baadhi yao wanalazimika kutumia kukusanya malipo kwa kutumia stakabadhi zinazo andikwa na mkono badala ya mashine za kieletroniki .
Kwa upande wake ,Diwani wa Kata ya Boma, Amir Nondo alishauri kuwa , ni vyema sheria zote ndogo za halmashauri zipitiwe upya na wakati zikipitiwa, sheria zilizopo bado zitaendelea kutumika hadi pale zitakazopitishwa na mamkala husika ya Tamisemi.
Akizunguzumia hoja hizo, Meya wa Manispaa hiyo alimwagiza Mkurugenzi kufuatilia suala la vikundi vya taka nguvu kuhusu kucheleweshewa asilimia ya malipo yao na pia kusimamia vyema mchakato utakaapoanza wa kupitiwa upya kwa sheria ndogo za halmashauri ili uwe ni shirikishi kwa wananchi kupitia madiwani wao.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa