Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro imeadhimisha siku ya mtoto wa Afrika inayoazimishwa Afrika nzima kila ifikapo tarehe 16 Juni lengo ikiwa ni kukumbuka mauaji ya watoto yaliyofanyika huko SOWETO Afrika ya kusini mwaka 1976. Chimbuko la Maadhimisho haya ni Azimio lililopitishwa na uliokuwa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU) mwaka 1990
Wanafunzi zaidi ya 10,000 waliandamana kupinga elimu duni na ya kibaguzi ya wakoloni ambapo wanafunzi 176 waliuawa katika maandamano hayo na mauaji hayo yalileta majonzi makubwa katika bara letu na kusababisha kuwepo kwa siku hii ili kupinga vikali ukatili dhidi ya watoto na kuhakikisha wanalindwa na kupatiwa haki stahiki.
Akisoma risala mbele ya mgeni rasmi Mhe Regina Chonjo Mkuu wa Wilaya ya Morogoro mtotoMichael Zungu ameeleza kuwa siku ya mtoto wa Afrika inawakumbusha watoto hatua ya kijasiri waliyoichukua watoto wenzao huko Afrika Kusini katika kulinda haki zao.Hatua hiyo imeonesha kuwa watoto wanaweza kuleta mabadilko hata wakiwa na umri dogo,hivyo siku hiyo uadhimishwa kwa maslahi mapana na kuwakumbusha wazazi/wazazi,wadau na serikali kushughulikia changamoto zinazowakabili ipasavyo.
Aidha alieleza kuwa watoto wanaishukuru Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kwa kuwathamini sana watoto kwa kufanya jitihada katika kuhakikisha haki za watoto zinalindwa na kutekelezwa katika ngazi zote na kwa kwa kuhakikisha hili Manispaa imeunda mabaraza ya watoto kuanzia ngazi ya mtaa,kata na Manispaa.
Pia Manispaa imeunda kamati za ulinzi na usalama za wanawake na watoto katika kata 29 na kamati hizi zimekuwa zikielimisha jamii juu ya haki za wanawake na watoto pamoja na kuzilinda,alisema Zungu.
Aidha ameeleza kuwa watoto wa Manispaa ya Morogoro bado wanapitia changamoto mbalimbali zikiwemo za vitendo vya ukatili wa kimwili,kihisia,kiuchumi na kingono katika mazingira wanayoishi hivyo ameiomba serikali kwa kushirikiana na wadau kuendelea kukemea vitendo vya dhidi ya watoto na hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi yao.
Kauli mbiu ya siku ya mtoto wa Afrika mwaka huu ni "MTOTO NI MSINGI WA TAIFA ENDELEVU,TUMTUNZE,TUMLINDE NA KUMUENDELEZA.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa