Waziri wa Nchi , Ofisi ya Rais ,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Suleiman Jafo ameupongezaUongozi wa mkoa wa Morogoro kwa kutekeleza vizuri ujenzi wa SokoKuu la kisasa linalojengwa katika Halmashauri ya Manispaa yaMorogoro.
Waziri Jafo alisemahayo baada ya kukagua ujenzi wa soko la kuu la kisasa laManispaa hiyo Februari 23, mwaka huu (2019) nakuridhishwa na maendeleo ya ujenzi wake ambao hadi kukamilika kwakeutakuwa umegharimu kiasi cha Sh bilioni 17.6, fedha zilizotolea naSerikali kuu.
Licha ya kutoa pongezihizo aliwataka wakandarasi ya ujenzi huo ambao ni kampuni ya Nandhrakuendelea na kasi ya ujenzi na wasirudi nyuma ili ukamilike kwa mudauliopangwa.
Waziri Jafo alisema,katika awamu ya kwanza ya utekelezaji wa miradi yakimkakati ipatayo 22 nchini imepata fedha kiasi cha zaidi ya Shbilioni 147 ikiwemo na Manispaa ya Morogoro.
“ Ninyi Manispaa ya Morogoro mmeanzavizuri tofauti na sehemu nyingine ambazo kwenye utekelezaji wamiradi hii bado wapo kwenye mchakato wa manunuzi , amakila mtu anakuja na mkandarasi wake na hiyo ni kwa ajili ya kutakakupata asilimia kumi (10%)” alisema Waziri Jafo.
Kwa mujibu waWaziri huyo, miradi hiyo haihitaji watu ama viongozi waingizemaslahi yao binafsi ,kwa vile ni miradi inayotakiwa ijibu matatizoya wananchi katika halmashauri zao .
Hata hivyo alisema ,lengo laSerikali ya awamu ya tano ya Rais Dk John Magufuli ni kuziwezesha halmashaurikwenye ujenzi wa miradi ya kimkakati.
Waziri Jafo alisema , kwa kazinzuri inayofanywa na Halmashauri ya manispaa ya Morogoro, yuko tayari kupitishafedha za miradi mingine ya aina hiyo iwapo wataomba.
“kwa speed hii inayoendelea siodhambi watu kama ninyi kuwapa mradi mwingine, sio dhambi” alibainisha Waziri Jafo.
Alisema , azma hiyoinalenga kutaka kuziona halmashauri zinatengeneza mifumowa kujiimarisha katika uwekezaji wa miradi mbalimbaliya maendeleo itakayochangia ukusanyaji wa mapato ya ndani.
“ Halmashauri zishindanekatika hali ya kujitegemea ili kuepuka utegemezi na kujitegemeakokote lazima uwe na vitega uchumi kama hivi vya soko” alisema na kuongeza.
“ Imefikia mahalipengine posho za mwezi za madiwani wanakopwa kutokana na halmashaurikuwa haina fedha” alisisitiza Waziri Jafo.
Naye Meya wa Manispaa ya Morogoro,Pascal Kihanga alimpongeza Rais kwa kuiwezesha kifedha halmashauri hiiili kujenga soko kuu la kisasa ambalo litachangia kujibu kiuya wafanyabiashara na kuiingizia mapato halmashauri.
“ Natoa shukrani kwa niaba yawananchi wa Manispaa kwa Serikali ya Mhe Rais Dk JohnMagufuli kwa kutoa fedha kwa ajili ujenzi wa miradi ya maendeleo ukiwemo wasoko hili” alisema Kihanga .
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa waMorogoro, Dk Kebwe Stephen Kebwe pamoja na kupokea maelekezo yaliyotolewana Waziri alimueleza kuwa tayari kuna miradi ambayo imeshaanzakuibuliwa ukiwemo na halmashauri hiyo ukiwemowa machinjio kwa lengo hilo la kutaka kujitegemeakimapato.
Awali , Mchumi kutoka ofisi yauchumi, Jacqueline Mushi katika taarifa yake kwa Waziri alisema,halmashauri ilitengewa kiasi cha Sh bilioni 10 kutoka wizara ya Fedha naMipango kwa ajili ya ujenzi wa soko hilo, huku halmashaurikupitia mradi wa uboreshaji wa Mjini (ULGSP) itachangia Sh bilioni 7.5 nakuufanya gharama za mradi kuwa ni Sh: 17.6
Mushi alisema , hadi sasamkandarasi wa ujenzi ameshalipwa Sh bilioni 3.8 na hatuaya utekelezaji wa mradi kwa ujumla kwa ujenzi wa jengo umefikia asilimia 30. 56na hatua ya ujenzi kwa mradi wote umefikia asilimia 22. 92 , ambapo mradi huoumepangwa kukamilika Septemba mwishoni mwaka huu.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa