Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kwa mwaka wafedha wa 2019/2020 inakisia kukusanya kiasi cha Sh 6,308 ,182,527.15 kutokakwenye vyanzo vyake vya ndani.
Licha ya kukisia kukusanya kiasihicho kutoka kwenye vyanzo vyake vya ndani, pia inakisia kupokea kiasi cha Sh 71,733,620,681.50kutoka vyanzo vya halmashauri, mapato kutoka Serikali kuu na kutoka kwawahisani.
Meya wa Manispaa , Pascal Kihangaalisema hayo katika hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano maalumuwa bajeti ya mwaka wa fedha 2019/2020 uliofanyika Februari 6, mwakahuu kwenye ukumbi wa halmashauri mjini Morogoro.
Alisema , licha yakukisia kupokea mapato ya kiasi cha Sh bilioni 71 .7 kutoka kwenyevyanzo hivyo vya mapato ,halmashauri pia imelenga kuimalishaukusanyaji wa mapato ya ndani .
Kihanga alisema ,halmashauriina kisia kukusanya kiasi cha Sh bilioni 6.3 ambapo niongezeko la Sh milioni 691 .8 ambayo ni sawa na asilimia 12.32 ya makadirio yamwaka 2018/2019 ya Sh bilioni 5.6
Meya wa Manispaa alisema , mapatohayo ya ndani yamelenga kutumia katika kupunguza kero za wananchi na kuwekakipaumbele kwenye utoaji wa huduma za elimu, maji, usafi wa mji ,utawala bora na Miundombinu.
Alisema, katika bajeti ya mwaka2018/2019 licha ya kupanga kukusanya kiasi cha Sh bilioni5.6, lakini iliweza kukusanya mapato halisi hadi kufikiaDesemba mwaka jana ( 2018) kiasi cha Sh bilioni 2.3 sawana asilimia 42.
Hata hivyo alisema ,katika mapatoyao, jumla ya kiasi cha Sh bilioni 3.1 zitatumika kwa ajili ya uchangiaji wamiradi ya maendeleo ikiwa ni sawa na asilimia 60 ya makisio.
Naye Mkurugenzi waManispaa, John Mgalula alisema ,ili kuongeza mapato yandani halmashauri imejiwekea mikakati mbalimbali ikiwa kupitia upyamifumo ya usimamizi na ufuatiliaji wa mapato kwa kuboresha maeneo ambayoyanamapungufu .
Pia alitaja mikakati mingine nikufanya ukaguzi wa mara kwa mara ili kubaini mianya inayovujisha mapato ,kutumia mifumo ya Ki- Elekroniki katika vyanzo vyote vya mapato ya ndani nakupitia upya sheria ndogo ya halmashauri za mapato ili ziendane na wakati.
Nao baadhi ya madiwaniwa baraza hilo kwa nyakati tofauti wakichangia hoja ya bajeti yaasilimia 60 ya maendeleo walimtaka mkurugenzi wa Manispaa kuhakisha fedhazinazotengwa zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa zikiwemo na fedha zaasilimia 10 ya makundi ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.
Pamoja na hilo , madiwani haowaliipongeza Serikali ya awamu ya tano kwa kuwezesha kutoa fedha za ujenzi wasoko kuu la Morogoro ambapo tayari ujenzi wake umeanza .
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa