MANISPAA ya Morogoro inategemea kukusanya kiasi cha Shilingi Bilioni 12.6 katika mwaka wa fedha 2022/2023.
Kauli hiyo imetolewa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga, katika Mkutano wa kawaida wa Mwaka wa Baraza la Madiwani uliofanyika leo Julai 19/2022, katika Ukumbi wa Mikutano wa Kilakala Soko Kuu la Chifu Kingalu Morogoro.
Mh. Kihanga ,amesema miongoni mwa vipaumbele katika mwaka wa fedha 2022/2023 ni makusanyo ya mapato, elimu, afya, usafi wa mji na utunzaji wa mazingira, utawala bora na mipango miji.
Kuhusu sekta ya afya, Mhe. Kihanga ,amesema mwaka wa fedha 2022/2023 watajikita katika kumalizia ujenzi wa kituo cha afya cha tungi na kumalizia miundominu ya Zahanati 4 ikiwamo Mji Mkuu, Kauzeni, Mafiga na Kihonda.
Aidha, upande wa sekta ya elimu, amesema Manispaa itajikita kumalizia ujenzi wa Maboma 50 ya madarasa ya Shule za Msingi, kujenga matundu 20 ya vyoo katika Kata ya Mlimani ikiwamo shule ya Msingi Mbete, na Towero, ujenzi wa majengo ya Utawala katika shule za Sekondari 7 (Mbuyuni, Tungi, Mazimbu, Mkundi, Kola Hill, Mafiga na Mwembesongo) na kuendeleza Ujenzi wa Shule Mpya ya Ghorofa iliyopo Kata ya Boma.
Katika upande wa mapato, amesema Manispaa inampango wa kununua mashine 150 za kukusanyia mapato na karatasi zake ( PoS).
Upande wa Mipango Miji, amesema , Manispaa itaendelea kugharamia fedha kwa ajili ya shughuli za Anwani za Makazi (Postcode),kuungua barabara za Kata na Mitaa kwa kushirikiana na TARURA.
Licha ya utekelezaji huo, Mhe. Kihanga, amesema ,Manispaa itaendelea kutoa mkopo wa asilimia 10 ikiwamo asilimia 4 ya Wanawake, asilimia 4 ya Vijana na asilimia 2 ya watu wenye ulemavu.
Naye Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Morogoro ambaye pia ni Afisa Tawala Wilaya, Hilary Sagara,amelipongeza Baraza la Madiwani pamoja na Menejimenti ya Manispaa kwa kazi nzuri ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo hususani kwa mwaka wa fedha 2021/2022.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Morogoro Mjini, Fikiri Juma, ameipongeza Manispaa ya Morogoro na kuwataka waendelee na umoja na mshikamano ili wafikie mara mbili ya walichokifanya katika mwaka wa fedha 2021/2022.
“SENSA KWA MAENDELEO ,JIANDAE KUHESABIWA TAREHE 23/08/2022”
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa