MANISPAA ya Morogoro imeanza vyema mashindano ya Shirikisho la Michezo Serikali za Mitaa (SHIMISEMITA), kwa kufanya vizuri katika michezo yake ya awali kwa timu ya mpira ya miguu, Netball naVollyball.
Katika mchezo wa awali wa mpira wa Miguu uliochezwa ,Manispaa ya Morogoro ilianza kwa sare ya kutofungana ya 0-0 dhidi ya timu yaTangaJiji.
Upande wa mchezo wa Netball, Manispaa ya Morogoro iliweza kuibuka na ushindi wa magoli 33 kwa 15 dhidi ya Timu ya Netball ya Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga.
Mchezo uliochezwa Oktoba 23/2022 ,Manispaa ya Morogoro upande wa mpira wa miguu ilifanikiwa kupata alama 3 za mezani kufuatia timu pinzani ya Halmashauri ya Hanang kutoingia uwanjani.
Na katika mchezo wa Volleyball ,Oktoba 23/2022, Manispaa ya Morogoro ilishinda jumla ya magoli 25 kwa magoli 12 dhidi ya Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga.
Katika mchezo wa leo mchana Oktoba 24/2022 ,Timu ya Manispaa upande wa Netball wataminyana dhidi ya Halmashauri ya Wilaya Ngara.
Mpira wa miguu, Manispaa leo Oktoba 24/2022 watachuana na timu ya Mpira wa Miguu ya Halmashauri ya Ifakara majira ya saa 7:00 mchana.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa