• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Morogoro Municipal Council
Morogoro Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
    • Wakuu wa Divisheni na Watumishi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Divisheni
      • Rasilimaliwatu na Utawala
      • Miundombinu, Uendelezaji wa Vijijini na Mijini
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ugavi na Manunuzi
      • Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Fedha na Uhasibu
      • Taka Ngumu na Usafishaji
      • TEHAMA
      • Michezo, Sanaa na Utamaduni
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Mazingira
    • Miundombinu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao Vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyoisha
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Fomu ya Maombi
    • Waraka
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
  • Market
    • Market line 1
    • Maket line 2

MANISPAA YA MOROGORO YAENDELEA KUTOA MATIBABU BURE KWA WAZEE

Posted on: September 19th, 2022

MANISPAA ya Morogoro yaendelea kusimamia utoaji wa matibabu kwa Wazee bila malipo, upatikanaji wa dawa Hospitalini na uwepo wa dirisha maalum kwa ajili ya Wazee ili kuwaenzi na kuwaondolea usumbufu.

Kauli hiyo imetolewa hivi karibuni na Katibu wa Afya Manispaa ya Morogoro Bertha Mahanga ,akimwakilisha Mganga Mkuu wa Manispaa ya Morogoro kwa niaba ya Mkurugenzi wakati wa kugawa Vitambulisho katika Makao ya Wazee Fungafunga Kata ya Kichangani.

Aidha, Mahanga , amesema Manispaa ya Morogoro , itaendelea kutoa huduma kwa wazee pasipo kuchangia gharama za matibabu na kuboresha changamoto ambazo zimejitokeza katika utoaji wa huduma hiyo kwa kundi hilo.

"Sisi sote ni mashahidi wa utolewaji wa huduma za Afya bila malipo kwa Wazee wote,nitoe wito kwenu kufika kwenye vituo vya huduma za Afya vya Serikali ili kupatiwa huduma bila kuchangia gharama za matibabu"Amesema Mahanga.

Kwa upande wa Afisa Ustawi wa Jamii na Mratibu wa Wazee Manispaa ya Morogoro, Rehema Malimi, amewaomba Maafisa maendeleo ya jamii wa kila Kata kuwashauri wazazi ambao watoto wao wanaolelewa na wazee kuona umuhimu wa mtoto kuishi na mzazi ili kuwapunguzia majukumu.

Malimi, amesema kuwa Wazee wengi wameachiwa watoto na watoto wao au wajukuu.

Aidha,amesema Malezi ya watoto hao ni jukumu la wazazi wao hivyo ni vema tukawaelimisha watoto na wajukuu zetu juu ya umuhimu wa malezi ya Wazazi kwa watoto.

"Kwa kuwa kila Kata kuna Maafisa Ustawi wa Jamii niwaombe mfike ili wazazi hawa waweze kuwajibika kama Sheria ya Mtoto Na. 21 ya Mwaka 2009 inavyoelekeza".Amesema Malimi.

Mwisho, Malimi, amempongeza Rais Samia kwa kazi nzuri ya kusimamia huduma za afya hususani katika kuwajali Wazee katika suala zima la matibabu bure na kutoa shukrani kwa viongozi wa Baraza la Wazee Manispaa ya Morogoro kwa kazi nzuri wanayofanya ya kuwaunganisha Wazee katika kuhakikisha wanapatiwa mahitaji yao ya Msingi.

Naye Mwenyekiti wa Wazee Fungafunga, Mzee Joseph Kaniki, ameushukuru Uongozi wa Manispaa ya Morogoro kwa kutekeleza ugawaji wa Vitambulisho pamoja na hatua wanazoendelea kuzichukua katika kuimarisha Sekta ya afya hasa kwa wazee.

Hivyo, Mzee Kaniki, amezidi kuchukua nafasi ya kumuombea Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan afya njema ili aweze kuiongoza vyema Tanzania katika kufikia maendeleo.

Katika utoaji wa Vitambulisho kwa Wazee wa Fungafunga, jumla ya Wazee 21 wamepigwa picha bure na kukabidhiwa Vitambulisho vyao vya msamaha wa matibabu.

Matangazo

  • TANGAZO LA MAPOKEZI YA MBIO ZA MWENGE WA UHURU MWAKA 2023 May 12, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI September 06, 2022
  • TANGAZO LA UUZWAJI VIWANJA ENEO LA KIEGEA A NA B December 02, 2022
  • ZABUNI YA UPANGISHAJI ENEO LA ROCK GARDEN MANISPAA YA MOROGORO August 16, 2022
  • Angalia Yote

Habari Mpya

  • RC MWASSA AITAKA JAMII KUJENGA MIFUMO BORA YA MALEZI.

    May 16, 2023
  • MWENGE WA UHURU WAPITISHA KWA KISHINDO MIRADI YA MANISPAA MOROGORO

    May 13, 2023
  • PAZIA LA MASHINDANO YA UMISSETA MANISPAA YA MOROGORO LAZINDULIWA MEI 11/2023

    May 11, 2023
  • MANISPAA YA MOROGORO YAZINDUA MASHINDANO UMITASHUMTA

    May 10, 2023
  • Angalia Yote

Video

MEYA KIHANGA AKABIDHI TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI ZAIDI YA 1600 WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Leseni za Biashara
  • Sheria Ndogo za Manispaa ya Morogoro
  • Sisi ni Nani

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Tamisemi
  • Morogoro Modern Market system (outside)
  • Tovuti ya Utumishi
  • Morogoro Modern Market System (LAN Network)
  • Tovuti Rasmi ya Ikulu
  • Tovuti ya RAS Morogoro

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro

    Anuani: 166 morogoro

    Simu: 0232614727

    Simu: 0734-039300

    Baruapepe : info@morogoromc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa