HALMASHAURI ya Manispaa ya Morogoro imefurahishwa na usimamizi wa shughuli za dampo la kutupia taka ngumu katika Jiji la Mbeya.
Kauli hiyo imetolewa na Meya wa Manispaa ya Morogoro Mh. Pascal Kihanga, katika ziara ya mafunzo ya kujifunza usimamizi wa miradi ya maendeleo na ukusanyaji wa mapato.
Akizungumza mara baada ya ziara kukamilika, Mhe. Kihanga, amesema usimamizi wa dampo ambao unafanywa na Jiji la Mbeya umekuwa wa kisasa na wenye lengo la kuhakikisha kuwa Jiji linakuwa safi masaa 24.
“Kuna mambo makubwa tumejifunza kwa wenzetu wa Jiji la Mbeya, wenzetu kwenye usafi wametuacha mbali sana , kuanzia uzoaji wa taka, ukusanyaji wa mapato, wenzetu wamejikita sana kulinda dampo la taka na kulisimamia lakini kuhusu ukusanyaji wa taka wameviachia vikundi kazi na makampuni jambo ambalo kwetu sisi tumebakia kusimamia dampo na ukusanyaji wa taka , kuna cha kujifunza tutakaa na wataalamu wangu na madiwani tutaona na sisi namna ya kuboresha ili Mji wetu ambao ni Jiji tarajiwa liwe safi kama ilivyo kwa wenzetu wa Jiji la Mbeya” Amesema Mhe. Kihanga.
Mhe. Kihanga,amesema Manispaa ya Morogoro imeshaanza ujenzi wa Dampo la kisasa ambapo amesema dampo hilo linakidhi matakwa yote ya kiafya na kimazingira, ”Sanitary Landfill’.
Kihanga,amesema Uendeshaji wa madampo kwa teknolojia ambayo Manispaa inakwenda kulitekeleza hutumika sehemu nyingi duniani hususan katika nchi zinazoendelea.
Kwa upande wa Kaimu Afisa Mazingira Manispaa ya Morogoro, Alex Roman,amesema uchafuzi wa mazingira kwa maji machafu yanayotirikika ambayo husababishwa na kujichuja kwa taka hizo (Leachate) ni sehemu ya changamoto zinazoikabili Manispaa ya Morogoro katika eneo ambalo dampo lipo kwa sasa.
Roman, amesema ili kukabiliana na tatizo hilo, manispaa ya Morogoro imeamua kujenga Dampo la Kisasa lenye eneo maalumu la kutupa taka(Cell) na bwawa la kuhifadhi maji machafu yanayotokana na kujichuja kwa taka (Leachate pond).
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa