Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro inatarajia kukusanya jumla ya Sh bilioni 6.4 kutoka vyanzo vyake vya ndani katika bajeti ya mwaka wa fedha wa 2018/2019 ambapo asilimia 60 ya mapato hayo yakielekezwa kutekeleza miradi ya maendeleo ya wananchi.
Meya wa halmashauri ya Manispaa , Pascal Kihanga alisema hayo ( Jan 15/01/2018) kwenye kikao maalumu cha baraza la madiwani kupitia na kupitisha bajeti ya fedha kwa mwaka 2018/2019.
Kihanga alisema ,halmashauri inakisia kukusanya na kupokea mapato kiasi cha Sh 74,801,384,234 kutoka kwenye vyanzo vya mapato toka Serikali kuu, wahisani na pamoja na vyanzo vyake vya ndani.
Hata hivyo alisema, bajeti ya mwaka 2018/2019 imelenga katika kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani na kutumia kupunguza kero za wananchi na kuweka kipaumbele katika utoaji wa huduma za elimu, maji, usafi wa mji, utawala bora , afya na miundombinu.
Kwa mujibu wa Meya ,kiasi cha makusanyo ya fedha kutoka vyanzo vya mapato ya ndani kinachokisiwa kuwa ni Sh 6,473,910,373 ambayo pia ni pungufu la Sh 367,280,668 sawa na asilimia 5.6 ya makadiriko ya mwaka wa fedha wa 2017/2018 ya Sh 6,841,191 , 045 . 05.
Alisema, katika mapato hayo, jumla ya Sh 3,415,109,624 zitatumika kwa ajili ya uchangiaji wa miradi ya maendeleo ikiwa ni sawa na asilimia 60 ya makisio.
Kihanga alitaja kiasi kingine cha Sh 44,232, 000, zitalipa mishahara kwa watumishi wasiopata ruzuku , Sh 2,276,739,749 kwa matumizi mengineyo na Sh 737,829,000 zitatumika katika Vituo vya Afya na Zahanati kupitia Mifuko ya utoaji huduma za afya.
Pia alisema , makisio ya mapato ya miradi ya maendeleo kwa mwaka 2018/2019 , halmashauri inakisia kupokea ruzuku kutoka serikali kuu na wahisani mbalimbali kiasi cha Sh 16,279,095,274 .Katika kiasi hicho, Serikali kuu inatarajia kutoa Sh 5,740,294,000 wakati wahisani wa maendeleo (ULGSP) kutarajiwa kutoa kiasi cha Sh 10,538, 538,801,274.
Naye Mbunge wa Jimbo la Morogoro mjini, Abulaziz Abood pamoja na kupitishwa kwa bajeti hiyo aliwataka watendaji wa halmashauri na madiwani wote kuwa na ushirikiano wa pamoja katika kusimamia utekelezaji wa miradi na malengo yaliyowekwa ili kuboresha huduma za wananchi.
Kwa upande wake , Diwani wa Kata ya Bigwa, Zamoyoni Abdallah aliwashauri madiwani wenzake kuwahamasisha wananchi kwenye kata zao hasa wanawake na vijana ili washiriki kuanzisha vikundi vya ujasiriamali wa viwanda vidogo waweze kunufaika na mikopo inayotolewa kwa ajili ya kuinua mitaji na kuwaondolea umaskini wa vipato.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa