MANISPAA ya Morogoro, imekabidhi jumla ya Kompyuta za mezani 30 kwa shule tatu 3 za Sekondari Mafiga, Kihonda na Kingolwira pamoja na Photokopi Mashine 2 kwa Vituo vya mafunzo vya TRC Kikundi na Kiwanja cha Ndege.
Tukio hilo la makabidhiano limefanyika Mei 02/2022 ambapo Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Pili Kitwana amekabidhi huku ikishuhudiwa na Afisa Elimu Msingi Manispaa ya Morogoro Chausiku masegenya , Afisa Elimu Vifaa na Takwimu Sekondari Anna Lupiano pamoja na Afisa TEHAMA Manispaa Zenna Lutego.
Akikabidhi kompyuta hizo, Kitwana, ameishukuru Lanes kwa msaada huo huku akibainisha kuwa lengo la Manispaa ya Morogoro ni kuwa Manispaa ambayo ipo kiganjani ambao taarifa yoyote inaweza kupatikana muda wowote.
" Ninaamini kompyuta hizi zitawasaidia sana wanafunzi na walimu pia yapo mambo yatakayotatuliwa kupitia kompyuta hizi, ili sasa kuleta elimu bora, na kutengeneza wasomi wazuri ambao watachangia katika uchumi wa Taifa letu" Amesema Kitwana.
Kitwana, amesema vifaa hivyo vimetoka Wizara ya Elimu kupitia ufadhili wa Lanes.
Naye , Afisa Elimu vifaa na Takwimu Manispaa ya Morogoro, Anna Lupiano, amewataka Waalimu kuwa makini na vifaa hivyo na wavitumie kwa matumizi yaliyokusudiwa.
Kwa upande wa Afisa TEHAMA Manispaa ya Morogoro, Zenna Lutego, amewataka Waalimu hao kuvitunza vifaa hivyo ili vizidi kuwasaidia baadae.
" Hivi ni vitu vya msaada , wenyewe siku wakija pengine wakahitaji kuviona vifaa hivi , sasa tukivitumia bila uangalizi vikaharibika tutapoteza uaminifu na misaada mengine tunaweza kuikosa" Amesema Lutego.
Nao Wakuu wa shule hizo 3 zilizopata Kompyuta, wakiwakilishwa na Mkuu wa Shule ya Sekondari Mafiga , Mwl. Robert Marwa, wameishukuru Manispaa ya Morogoro kupitia Wizara ya elimu kwa kuwasaidia kompyuta hizo na kueleza namna zitakavyowasaidia.
"Kompyuta hizi kwanza zitatusaidia kuwezesha mawasiliano hususani katika masuala ya intaneti kwa ajili ya kutuma na kupokea taarifa mbalimbali kwa wakati na kuchapa majaribio ya wanafunzi , lakini vifaa hivi vitasaidia sana wanafunzi kujifunzia kwa vitendo wawapo shuleni na kutafuta 'notes' za masomo mbalimbali ili waweze kujifunza"
" Amesema Marwa.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa